WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kufyekelea mbali ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma katika taasisi za elimu ya juu nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Akizungumza mbele ya Rais John Magufuli leo tarehe 27 Novemba 2018 jijini Dar es Salaam, Prof. Ndalichako amesema kuna baadhi ya watu wanajificha nyuma ya taaluma zao kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
“Baadhi ya watu wanataka kujificha nyuma ya taaluma kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma, ukiukwaji wa maadili ya utumishiwa umma tutaufyekelea mbali,” amesema Ndalichako.
Aidha, Prof. Ndalichako amesema serikali itahakikisha taasisi za elimu ya juu zinakuwa mfano wa kuigwa kwa taifa letu ikiwemo kwa kufuata sheria na maadili ya utumishi wa umma.
Leave a comment