PANGUAPANGUA ya Utawala wa Awamu ya Tano imeshika kasi ambapo leo jijini Dar es Salaam Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi amesitisha mkataba wa kazi wa George Nyatenga, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, anaandika Mwandishi Wetu.
Pamoja na hatua hiyo, Prof. Ndalichako amewasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa bodi hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali.
Waliosimamishwa ni Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala; Juma Chagonja, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.
Hata hivyo, Prof Ndalichako amemwagiza mkaguzi wa ndani kuhakiki maelezo na nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa.
More Stories
Rais Mwinyi ateua mrithi wa Maalim Seif
Rais Mwinyi: Nileteeni anayefanana na Maalim Seif
Jina la mrithi wa Maalim Seif, lafikishwa kwa Rais Mwinyi