BAADA ya kupachika bao lake baada ya mwaka mmoja na siku 52 kupita, mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa alikuwa anaumia wakati alipokuwa hafungi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Nchimbi amefunga moja ya bao katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata Yanga dhidi ya Gwambina FC kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baada ya mchezo huo kukamilika, Nchimbi alisema amejisikia furaha kwa kupachika bao hilo na alikuwa anaumia kuona hafungi katika michezo aliyokuwa anacheza.
Kwenye mchezo wa leo Nchimbi alipachika bao hilo kwenye dakika ya 18 ya mchezo.
Mara ya mwisho Nchimbi kufunga ilikuwa kwenye ushindi wa mabao 3-0, kwenye mchezo dhidi ya Alliance FC, tarehe 29 Februari 2021.
Leave a comment