BAADA ya kupita mwaka mmoja na siku 52, hatimaye mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi amefanikiwa kupachika bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Nchimbi amepachika bao hilo kwenye dakika ya 18 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mara ya mwisho Nchimbi kupachika bao akiwa na jezi ya Yanga ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Alliance uliochezwa Februari 29, 2020, ambapo alipachika mabao mawili akitokea benchi.
Hili litakuwa bao lake la kwanza toka kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2020/21.
Leave a comment