Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya ‘Nchi zenye sifa hizi Afrika, zipo hatarini kwa corona’
Afya

‘Nchi zenye sifa hizi Afrika, zipo hatarini kwa corona’

Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge Kenya
Spread the love

NCHI ambazo zinahifadhi wakimbizi wengi na zenye makazi duni Afrika, zinatajwa kuwa na hatari zaidi ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) katika siku za usoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge nchini Kenya, ametaja nchi ambazo iwapo hatua kali hazitachukuliwa, zinaweza kujikuta kwenye hatari zaidi ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania.

Na kwamba, nchi hizo baadhi zina idadi kubwa ya wakimbizi ambao wamewekwa pamoja, lakini pia yapo maeneo wakazi wake wamefungamana na kuwa hatari zaidi katika kuenea kwa ugonjwa huo ikiwemo Kibera, Kenya.

Pia amesema, maeneo yaliyo na vita na majanga mengine ikiwemo Sudani Kusini, yamo kwenye hatari kubwa ya ugonjwa huo, hivyo akishauri hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukabili virusi hivyo.

“Nchi zilizo katika Jangwa la Saharan, kwa sasa zina kesi za maambukizi zaidi ya watu 1,300 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

“Hasa nchi ambazo zinahifadhi wafungwa wengi na makazi duni ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania,” anasema.

Katika taarifa yake aliyoitoa tarehe 25 Machi 2020, Derbyshire anasema, mji wa kibera uliojitenga, una hatari zaidi kutokana na mazingira yake duni yanayotokana na kukosa maji safi, sabuni na vituo bora vya afya.

“Tumeona namna ambavyo nchi zilizoendelea kwa kiwango kikubwa katika masuala ya afya, zinataabika. Ni rahisi kujua sasa kwa kiwango gani corona inavyoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha janga duniani, wazee ndio wanaotaabika sana,” amesema Derbyshire.

Anasema, watu wenye umri mkubwa ndio wameathirika sana na corona, na wameathirika zaidi kutokana na kinga zao kuwa na uwezo mdodogo – dhaifu.

Hivyo amesema, hatari zaidi ni kwa watu wenye umri mkubwa wanaoishi katika mazingira magumu ya upatikanaji hafifu wa chakula, maji na huduma za afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!