November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nchi tisa Barani Ulaya zafuzu kombe la Dunia

Spread the love

 

MATAIFA tisa kutoka Barani Ulaya, yameafanikiwa kufuzu moja kwa moja kwenye michuano ya kombe la Dunia, mara baada ya kumalizika vinara kwenye makundi yao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Michuano hiyo ya 32, ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia ‘FIFA’ itachezwa Juni, Mwakani nchini Qatar.

Jumla ya mataifa 55, ambayo yaligawanywa kwenye makundi 10, na kundi moja kuwa kati ya timu tano au sita na patashika hizo zilianza kuchukua nafasi kuanzia Machi 2021, kwa kutafuta wawakilishi 13, watakaowakilisha bara hilo kwenye michuano hiyo.

Makundi tisa mpaka sasa yameshakamilisha michezo yao na kupata wawakilishi watakaokwenda moja kwa moja, huku kundi … likitarajiwa kukamilisha michezo yao hapo baadae na timu ya Taifa ya Uholanzi ikiwa kinara kwenye kundi hilo, licha ya kutokuwa na uhakika wa kufuzu mpaka sasa.

Timu zilizofuzu mpaka sasa ni Ujerumani ambaye alimaliza kinara kwenye kundi J, Croatia, Dernmark, Ubeligiji, Ufaransa, Hispania, England na uswiss.

Kufuatia timu 10 kufuzu moja kwa moja na kusalia na nafasi tatu, jumla ya timu sita ikiwemo Itary na Ureno zitacheza mchezo wa mtoani (Playoff) kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ili kukamilisha idadi ya timu 13.

 

error: Content is protected !!