August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nchi 165 kujenga historia mpya

Spread the love

ZAIDI ya nchi 165 zinatarajiwa kuingia mkataba wa kihistoria wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye hafla inayofanyika leo mijini New York nchini Marekani, anaandika Regina Mkonde.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Idara ya Habari ya Umma ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa mkataba huo utasainiwa ili kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa katika kikao kilichofanyika Desemba mwaka jana mjini Paris, Ufaransa ambapo mwenyeji wa hafla hiyo ni Ban Ki-moon.

Uingiaji saini katika mkataba huo utakuwa wa kihistoria kutokana na kwamba, kumekuwa na ongezeko kubwa la nchi zitakazosaini mkataba huo toka ilivyotokea mwaka 1982 ambapo nchi 119 zilisaini mkataba wa sheria ya bahari.

Kati ya nchi zitakazosaini mkataba huo leo, ni pamoja na nchi zenye uchumi mkubwa duniani na zile zinazoongoza kwa kuzalisha hewa chafu.

Kusainiwa kwa mkataba huo ni hatua ya kwanza  kuelekea kuhakikisha kwamba mkataba unaanza kufanya kazi yake haraka iwezekanavyo, vile vile kila nchi itakayosaini italazimika kukubali au kuridhia matakwa ya mkataba huo.

Katika hafla hiyo msichana wa kitanzania Gertrude Clement (16) atashughulikia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Watakaosaini mkataba huo ni wakuu wa nchi au serikali, mawaziri wanje au wawakilishi wengine na mamlaka rasmi kutoka katika serikali iliyothibitisha kusaini makubaliano hayo.

error: Content is protected !!