July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nchemba: Nitafukuza wala rushwa

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na mke wake Neema Mwigulu wakifurahia kukabidhiwa kwa fomu za kugombea urais.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na mke wake Neema Mwigulu wakifurahia kukabidhiwa kwa fomu za kugombea urais.

Spread the love

HEKAHEKA za makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimeshika kasi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Leo Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba amefungua pazia la uchukuaji fomu na kuahidi kufukuzwa wala rushwa wote katika utawala wake.

Akiongozana na mke wake, Mwigulu baada ya kukabidhiwa fomu, alikutana na waandishi wa habari kwa lengo la kuulizwa maswali.

Kabla ya kuulizwa maswali Mwigulu amesema, akipata ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha anakuza uchumi wa nchi kwa kufufua viwanda na kuendeleza kilimo bora na kilicho na tija.

Pamoja na hivyo amesema, rasilimali za nchi atazitumia vizuri ile ziwe neema kwa watanzania wote ikiwa ni sambamba na kukomesha matumizi mabaya ya fedha.

“Katika uongozi wangu, nitakomesha kabisa matumizi mabaya ya fedha na ikionekana viongozi au kiongozi amehusika katika hilo, atafukuzwa na kufilisiwa mali zote.

 “Kwanini kuwe na matumizi mabaya ya fedha wakati kuna mambo muhimu hatujayakamilisha. Kuna shida ya madawati mashuleni, madawa hosptalini, nitapambana na matumizi hayo ili kuboresha sehemu husika.” Amesema Mwigulu.

Katika awamu yake amesema, atapambana na tatizo la ajira kwa vijana kwa kufufua na kuanzisha viwanda vingi hali itakayochochea ongezeko la ajira nchini.

Amefafanua kuwa, katika awamu yake atapambana na rushwa na ikibainika mtumishi wa umma anapokea au kutoa, atamfukuza madarakani.

Akijibu maswali ya waandishi lilihoji endapo akifanikiwa kuwa Rais atalidhibiti vipi deni la Taifa .

Amesema, deni hilo  limekuwa kwa kasi kubwa kipindi cha uongozi wa Awamu ya Nne na hiyo yote ni kutokana na kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo zaidi ya 200.

 Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barbara, bomba la gesi na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Aliyefuata kuchukua fomu mjini hapa ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Mussa Mwapongo.

Mwapongo amesema, hakuja kuongea isipokuwa ni kuchukuwa fomu tu na kwamba atazungumza na waandishi kesho jijini Dare es Salamu.

Hata hivyo amesema, hana shaka na CCM kwani kina demokrasia na utamaduni mzuri ambapo kinatoa nafasi kwa kila mwanachama anayedhani ana uwezo katika kuwania nafasi hiyo kubwa.

 Mwapango alishauri wagombea mwengine kwenda kuchukua fomu na kuwataka kutokatishwa tamaa kwa namna yoyote na badala yake wasikilize sauti zitokazo mioyoni mwao.

error: Content is protected !!