January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NCCR yatoa msimamo kuhusu Zanzibar

Spread the love

BAADHI ya viongozi wa siasa nchini wametaka wigo wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibari upanuliwe kwa kushirikisha wadau wote baada ya kuviachia vyama vinavyovutana vya CCM na CUF peke yao. Anaandika Eunice Laurian …. (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametaka mgogoro huo kutatulia kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar  pamoja na kuhusisha kituo cha demokrasia nchini ili kupata suluhusu ya suala hilo.

“Meza ya mazungumzo ndio suluhisho la amani duniani kote na ndiyo utaratibu wa dunia, wanasiasa ndiyo wanatakiwa kukaa pamoja kumaliza mgogoro wa Zanzibar na si vinginevyo,” alisema Mbatia.

Mbatia amesema kuwa mgogoro huo wa kikatiba usipotatuliwa na kuwafuata busara ya kuwahusisha wadau tofauti unaweza kusababisha machafuko visiwani humo na kuliharibia jina taifa pamoja na kugharimu maisha ya watanzania.

Alisisitiza haja ya kupitia kwa makini hoja zilizotolewa na ZEC kupata ufumbuzi wa kudumu, alisema mgogoro wa Zanzibar utatuliwe kwa maridhiano ya kisiasa kati ya Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Sharif  Hamad.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha sauti ya Umma (SAU), Yusuph Manyanga amesema kuwa majadiliano ya vyama viwili kwa sasa haya lengi kutafuta suluhisho kutokana na kila chama kuvutia upande wake.

error: Content is protected !!