June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NCCR wataja mgombea wao urais

Mwenyekiti wa kitengo cha vijana wa NCCR- Mageuzi, Deo Meck (katikati) akizungumza na waandishi wa habari

Spread the love

CHAMA cha NCCR- Mageuzi, kimemtangaza Dk. George Kahangwa, mkuu wa idara ya itikadi na uenezi wa chama hicho, kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwaka huu. Anaandika Pendo Omary… (endelea).

Mwenyekiti wa kitengo cha vijana wa NCCR- Mageuzi, Deo Meck amewaambia waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kuwa Kahagwa, ndiye aliyependekezwa na chama chake kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ngazi ya chama muda ukifika.”

“Kwa kuzingatia kila kizazi na kila msimu unaweza kuwa na mahitaji yake, NCCR- Mageuzi imeamua kumsimamisha Dk. Kuhangwa katika nafasi ya urais,” ameeleza Meck.

Anasema, mgombea huyo wa NCCR- Mageuzi, atashindwa na wagombea wengine wa vyama vinavyounda Muungano wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA), ili apatikane mgombea mmoja atakayewakilisha vyama hivyo.

UKAWA inaundwa na vyama vya Chadema, NCCR- Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na National League Democrat (NLD). 

Hata hivyo, Meck amedai kuwa uamuzi wa kumisimamisha Dk. Kuhangwa, siyo msimamo wa chama; vikundi vingine havikatazwi kutangaza mtu mwingine wanayedhani anafaa kugombea urais.

“Sisi kama vijana hatuna maamuzi ya mwisho. Katiba ya chama inaturuhusu ndani ya vitengo kupendekeza au kushawishi watu kugombea. Hivyo tunachokifanya ni kumshawishi Dk. Kahangwa agombee nafasi hiyo ndani ya chama. Ila chama ndicho kina maamuzi ya mwisho ya nani atapeperusha bendera ya NCCR-Mageuzi ndani ya UKAWA,” amesema Meck.

Aidha, akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, Dk. Kahagwa amesema kitendo cha kitengo cha vijana wa chama hicho, kutangaza kumshawishi kugombea nafasi hiyo ndani ya chama ni haki yao. Na vijana hao wanahaki ya kutumia fursa na rasilimali ikiwemo ofsi za chama katika shughuri za kisisa bila kuvunja katiba ya chama.

“Ni jambo linalonifanya nitafakari. Hata mimi nimesikia wametangaza hivyo. Wakija kunishawishi, nitazungumza nao. Kulingana na hoja watakazokuja nazo. Naweza kukubali au kutoa maamuzi mengine,” amesema Dk. Kuhangwa.

error: Content is protected !!