Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR-Mageuzi yawaonya wanaokibeza, kudhoofisha upinzani
Habari za Siasa

NCCR-Mageuzi yawaonya wanaokibeza, kudhoofisha upinzani

Edward Sembeye, Mkuu wa Mawasiliano ya Umma NCCR-Mageuzi
Spread the love

TUHUMA za kutumika katika kudhoofisha vyama vya upinzani nchini Tanzania, hususan katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, zimekiibua Chama cha NCCR-Mageuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tuhuma hizo zimeibuka hivi karibuni, kufuatia wimbi la baadhi ya wabunge  na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kujiunga nacho, huku wakitoa tuhuma nzito dhidi  ya viongozi wa chama walichotoka.

Leo tarehe 28 Mei 2020, Edward Sembeye, Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi Taifa, amesema si za kweli, bali  ni muendelezo wa propaganda na siasa chafu dhidi ya chama hicho.

Sembeye ametoa kauli hiyo kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa umma, kuhusu msimamo wa NCCR-Mageuzi, juu ya watu wanaotangaza kujiunga na chama hicho na orodha ya wanasiasa mbalimbali waliokwisha kuhama vyama vyao.

“Wakati sisi tunaendelea kuheshimu demokrasia ya vyama vingi kwa kiasi hicho, wapo watu ambao, kwa sababu wanazozijua wao, wanakipaka matope chama chetu pindi kinapopokea mwanachama mpya. Mathalani, kuna uzushi kuwa watu hao wananunuliwa ,” amesema Sembeye

“Wapo pia wanaozua kuwa, wanaojiunga nasi wamepewa maagizo kutoka nje ya chama, waje NCCR- Mageuzi. Wanaotamka hayo, si tu wanatukosea adabu, bali wanawavunjia heshima watu wanaotumia haki na uhuru wao wa kikatiba.”

Sembeye amewataka watu wanaotoa tuhuma hizo dhidi ya chama chake, kuacha mara moja, kwa kuwa hazitakirudisha nyuma chama hicho, katika harakati zake.

“NCCR-Mageuzi tunawataka wazushi hao waache upuuzi huo ambao sisi ndani ya chama tunaziita propaganda za maji taka. Uongo na uzushi wao, kamwe hautarudisha nyuma jitihada zetu wanamageuzi, na wala wasidhani zitawazuia watu kuendelea kuamini katika itikadi nzuri ya utu na kuchukua hatua ya kujiunga nasi,” amesema Sembeye.

Sembeye amesema mtu yeyote ana haki ya kuhama chama cha siasa, na kwamba NCCR-Mageuzi nacho kilikimbiwa na wanachama wake, lakini hakijawahi kuweka uhasama na vyama ambavyo wanachama wake walijiunga navyo.

“Mageuzi, ni miongoni mwa vyama vilivyowahi kuondokewa na wanachama wake huku wengine wakiendelea kujiunga. Maadam NCCR- Mageuzi, kupitia itikadi ya utu, tunaheshimu misingi ya uhuru na haki, hatujawahi kuwa na uhasama na yeyote kwa sababu kaondoka kwetu, wala hatumzuii mtu anayestahii kujiunga nasi, aingie katika chama chetu,” amesema Sembeye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!