Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR-Mageuzi wamgomea Jaji Mutungi
Habari za SiasaTangulizi

NCCR-Mageuzi wamgomea Jaji Mutungi

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Spread the love

 

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania cha NCCR-Mageuzi kimesema, hakitashiriki kikao kilichoitishwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na jeshi la polisi kwa kuwa “maandalizi yake hayakuwa shirikishi, jumuishi wala uwazi.” Anaripoti Ibrahim Yamola, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, watazungumza na wadau wa demokrasia na vyama vingine ambavyo ni wahanga wa matendo, uonevu na unyanyasaji ili kupata namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, tarehe 18 Oktoba 2021 na James Mbatia wakati akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya NCCR-Mageuzi, Ilala jijini Dar es Salaam.

Ni baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya chama hicho, iliyokutana jana Jumapili na kuazimia kwa pamoja kutoshiriki kikao hicho.

Ofisi ya msajili inayoongozwa na Jaji Francis Mutungi imeitisha kikao cha wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya siasa na jeshi la polisi kujadili namna bora ya kuendesha shughuli za kisiasa kitakachofanyika tarehe 21-23 Oktoba 2021, jijini Dodoma.

Akitoa sababu za kutoshiriki kikoa hicho, Mbatia amesema “ofisi ya msajili nao ni watuhumiwa katika hili. Sisi NCCR-Mageuzi tarehe 28 Agosti 2021, tulizuiwa kufanya kikao chetu cha kamati kuu, lakini msajili alikaa kimya. Sasa huyu mlezi anatuita kufanya nini kama ameshindwa kusimamia katiba na sheria?”

“Msajili huyu huyu Jaji Mutungi, aliomba vyama kusimama kufanya shughuli za siasa kupisha kuitisha kikao, lakini CCM wao wakafanya ziara mikoani ikiongozwa na katibu mkuu, Daniel Chongolo na msajili hajasema lolote.”

“Unajiuliza huyu msajili mbona anashindwa kusimamia katiba na sheria? Lakini tujiulize ni lini kikao, kongamano au shughuli yoyote ya CCM ambayo imezuiwa na polisi, hakuna ila ya kwetu inazuiwa na yeye anakaa kimya. Sasa tunakwendaje kwenye kikao ikiwa yeye mwenyewe haheshimu katiba na sheria,” amesema Mbatia

Mbatia alisema, hata kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kusema “mikutano ya vyama vya siasa isubiri kwani anajenga uchumi, hii ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi.”

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi

Mwenyekiti huyo amesema “Jeshi la polisi kufanya vitendo vya ubaguzi kwa baadhi ya vyama vya siasa, kwa kuzuia shughuli halali za kisiasa za kukutana, kujumuika na kujitangaza, hii ni kukiuka katiba na sheria.”

Mbatia amemwomba Jaji Mutungi kuwa “namheshimu sana kwa sababu anatumia jina la Francis la baba yangu. Lakini katika hili sikubaliana naye. Asimamie katiba na sheria.”

NCCR-Mageuzi, kinakuwa chama cha pili kuweka msimamo wa kutoshiriki kikao hicho kikitanguliwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, ambacho kilikwisha weza wazi kwamba hakitashiriki kikao hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!