Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR-Mageuzi: Rais Samia atafakari upya uamuzi wake
Habari za SiasaTangulizi

NCCR-Mageuzi: Rais Samia atafakari upya uamuzi wake

Edward Sembeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi
Spread the love

 

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania, NCCR-Mageuzi, kimemwomba Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan, kuufikilia upya uamuzi wake kuhusu suala la katiba mpya na mikutano ya hadhara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

NCCR-Mageuzi kimesema, suala la Katiba mpya ni takwa la wananchi linalopaswa kutekelezwa huku mikutano ya hadhara ipo kwa mujibu wa sheria hivyo inapaswa kuruhusiwa.

Hayo yamesemwa na Edward Simbeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, alipofanya mahojiano maalum na MwanaHALISI TV kuhusu siku 100 za utawala wa Rais Samia.

Rais Samia aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo, John Pombe Magufuli, kufariki dunia.

Mapema wiki hii, Rais Samia akizungumza na wahariri na waandishi wa habari Ikulu ya Dar es Salaam kuhusu siku 100, alisema suala la katiba mpya na mikutano ya hadhara, isubiri kwanza hadi aisimamishe nchi kiuchumi.

Fuatilia mahojiano kati ya MwanaHALISI TV na Simbeye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!