August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NCCR-Mageuzi kuvishtaki vyombo vya habari

Martha Chiomba

Spread the love

CHAMA cha NCCR-Mageuzi upande unaongozwa Haji Ambar Khamis umesema chombo cha habari kinachomtambua James Mbatia kama Mwenyekiti, watakishtaki. Anaripoti Faki Ubwa… ( endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 17Julai, 2022 na Katibu Mkuu wa Chama hicho Martha Chiomba wakati akizungumza na vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam.

Amesema wamesikia kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya Habari mbalimbali vya habari vikiendesha mahojiano na mmoja wa wanachama wao aliyejitambulisha kama mwenyekiti.

“Ikumbukwe kuwa vyombo vya Habari vinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya vyombo vya Habari na kwa sababu hiyo chama kitachukua hatua kwa chombo chochote kitachoendelea kugawa vyeo vya Chama chetu kiholela kwa mwanachama yeyote bila idhini ya Chama” amesema Chiomba.

Amesema chombo cha habari kinachomtambua Mbatia kama Mwenyekiti ilhali Halmashauri Kuu imemsimamisha Chama hicho kitakishtaki chombo hicho.

Amesisitiza kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia amesimamishwa uenyekiti na kutofanya shughuli zozote za chama mpaka pale mkutano mkuu maalum utakapoketi ili umhoji juu ya makosa yake .

Upande huo umemsimaisha uenyekiti Mbatia kwenye Mkutano uliotajwa kuwa ni wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kwa kukiingiza Chama kwenye migogoro.

“Vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea kufanywa na ndugu Mbatia na Kundi lake…anadharau uamuzi wa vikao halili vya chama” amesema Chiomba.

Chiomba amesema kuwa Mbatia na watu wake wanaendelea na vikao vya chama ilhali si viongozi jambo ambalo anajiongezea mashtaka mbele ya Kamati Kuu.

“Vitendo hivyo vinakifanya Chama kuendelea kuorodhesha makosa yake na kuwasilishwa kwenye vikao vya uamuzi wa Chama” amesema Chiomba .

Pia amesisitiza kwa wanachama wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali kutomtambua Mbatia kama kiongozi na kwamba ziara yake itakayoanza tarehe 15 isiungwe mkono.

Tarehe 21 Mei mwaka huu Halmashauri kuu ya chama hicho ikiongozwa na Mjumbe halmashauri hiyo, Joseph Selasini ilitangaza kumsimamisha uenyekiti Mbatia.

Hata hivyo, Mbatia alipinga kung’olewa na kudai mkutano huo ulikua batili licha Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kuutambua na kubariki maamuzi yake.

error: Content is protected !!