Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR Mageuzi Kahama waitaka Serikali itangaze uchaguzi mdogo wa mtaa
Habari za Siasa

NCCR Mageuzi Kahama waitaka Serikali itangaze uchaguzi mdogo wa mtaa

Sanduku la kura
Spread the love

 

CHAMA cha NCCR Mageuzi Kata ya Malunga Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kimeitaka serikali kuitisha uchaguzi wa marudio katika mtaa wa Igomelo kufuatia kusimamishwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa huo, Laurent Mollyanda ili kupata mwenyekiti mwingine. Anaripoti Paul Kayanda, Shinyanga … (endelea).

Katibu wa chama hicho Kata ya Malunga, Samir Sadiki akizungumza na waandishi wa Habari jana Ofisini kwake amesema kuwa kwa sasa wananchi wa mtaa huo hawana kiongozi ngazi ya mtaa huo kwa muda murefu sasa huku serikali ikilitazama suala hilo bila muafaka wowote.

Amesema amri ya kusimamishwa kazi kwa mwenyekiti huyo ilidaiwa kuwa ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika kwenye kata hiyo bila kutangaza kinyang’anyiro kingine kwa vyama vya siasa ili kupata mwenyekiti mwingine.

Katibu huyo wa chama alidai kuwa kutokana na muda wa ukomo wa mwenyekiti huyo, kiti hicho kimekuwa wazi kwa muda unaozidi miezi saba tangu tarehe 26 Oktoba, 2021 aliposimamishwa mpaka sasa.

Amesema chama kinaomba uchaguzi uitishwe mara moja ili wananchi wapate haki yao ya kikatiba ya kuchaguliwa ama kuchagua ili kuziba nafasi hiyo.

Akizungumza na Mwanahalisi Online aliyekuwa mwenyekiti wa Mtaa wa Igomelo, Laurent Mollyanda amesema tarehe 6 Novemba, 2021 Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Emmanuel Mloso alikuja ofisini kwake kuchukua vitendea kazi vyake kama mhuri wa serikali ya mtaa bila maelezo ya kina jambo ambalo lilisababisha wananchi kukosa huduma ya mwenyekiti wao.

“Mhuri ulichukuliwa na afisa mtendaji wa Kata na sijarejeshewa mpaka sasa na sina maelezo ya maandishi ya kunyang’anywa mhuri wa mamlaka yangu niliokabidhiwa baada ya ushindi kipindi cha mwaka 2019,” amesema.

Aidha, mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya kunyang’anywa mhuri ulikabidhiwa kwa mtu ambaye hajachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa utaratibu na sheria.

Pamoja na mambo mengine mwenyekiti huyo amedai kuwa amemwandikia barua afisa huyo mtendaji wa kata ya kuomba maelezo ya maandishi sababu kubwa iliyopelekea kujitwalia mhuri huo na kutoa siku saba awe amerejeshewa vinginevyo atarudi ofisini kwake kuendelea na jukumu la kuhudumia wananchi kama kawaida.

Hata hivyo, kwa mujibu wa barua yenye kumb.Na. KMC/MLNG/WEO11/2021/72 iliyosainiwa na afisa mtendaji huyo inatamka kuwa rejea agizo la mkuu wa Wilaya kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 26/10/2021 akiwa katika ziara ya kikazi kusikiliza na kujibu malalamiko ya wananchi.

Barua hiyo inatamka kuwa katika kikao hicho, mkuu wa wilaya aliagiza mwenyekiti wa mtaa wa Igomelo, Laurent Mollyanda kusimama ili kupisha tuhuma zilizowasilishwa na chama chake – CCM ikiwemo kutoa adhabu ya kumsimamisha uanachama kwa muda wa mwaka mmoja.

Barua hiyo inatamka kuwa inazingatia hayo na kuamuru kufanya makabidhiano na mtendaji wa mtaa nyaraka zote za ofisi alizokuwa anazitumia wakati wa uongozi wake ikiwemo mhuri ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shoinyanga Mabala Mlolwa alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alikana na kudai kuwa taarifa hizo hazijafika ofisini kwake na kuliomba gazeti hili lihoji ngazi za chini ili kupata ukweli wa Sakata hilo.

Hata hivyo, kwa upande wa Barua iliyosainiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba yenye Kumb.Na. KMC.AP.30/28/12 ikijibu madai ya chama cha NCCR Mageuzi inasema, utaratibu wa kumuondoa madarakani mwenyekiti wa mtaa umeainishwa kisheria katika kanuni zinazoelezea utaratibu wa kumuondoa madarakani wa mtaa huo Mwenyekiti wa Mtaa, Tangazo la Serikali Na.265 la Mwaka 1995.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!