January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NCCR chatangaza majimbo yake

Spread the love

CHAMA cha NCCR – Mageuzi kimetangaza majimbo 19 ambayo kitasimamisha wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Majimbo hayo ni kati ya majimbo 265 ya uchaguzi. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Nderakindo Kessy, amesema mpaka sasa chama hicho kina asilimia 86 ya wagombea huku wakitarajia kukamilisha idadi kamili muda wowote kuanzia sasa. 

“Baada ya mchakato wa maridhiano ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), NCCR – Mageuzi tumepata majimbo 19 ambayo ni Kasuru Vijijini, Kasuru Mjini, Buyungu, Muhambwe, Kigoma Kusini, Manyoni, Vunjo, Mwanga, Mufindi Kusini na Mbinga Mjini, ” amesema Kessy.

Kessy ameyataja majina mengine kuwa ni; Ileje, Serengeti, Gairo, Mpwawa, Kibakwe, Mtera, Mtwara, Mtwara Mjini, Mkenge na Ngara.

Aidha, Kessy amesema habari iliyoandikwa leo na gazeti la Uhuru yenye kichwa cha habari “Mpasuko UKAWA” si ya kweli na kwa sasa wapo kushughurikia taarifa hiyo ili kuona nini cha kufanya.

“Msemaji Mkuu wa chama ni Mwenyekiti wa chama, James Mbatia. Kauli hiyo haikutolewa na msemaji wa chama. Kuna kanuni zitatumika kutatua tatizo hili na tutatoa maamuzi muda mwafaka ukifika,”amesema Kessy.

Gazeti la Uhuru la leo limemnukuu Afisa Idara ya Kampeni na Uchaguzi ya NCCR – Mageuzi, Faustne Sungura akisema “uchu wa madaraka unaofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) utapelekea mgombea wake kunyimwa kura za urais.

error: Content is protected !!