January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NBS: Mfumko umeongezeka kwa 4%

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo

Ephraimu Kwesigabo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema, mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi  Mei  2015 umeongezeka kwa asilimia 04 ikilinganishwa na ongezeko la aslimia 08 ya mwezi Aprili mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Kwesigabo amesema, fahalisi za bei zimeongezeka hadi 167.86 mwezi Mei mwaka huu kutoka 157.21 mwezi Aprili, 2015.

Amesema, kuongezeka kwa fahalisi hizo kumechangiwa na  kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula.

Akitaja bidhaa za vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa fahalisi amesema, ni pamoja na mahindi kwa asilimia 3.3, unga wa mahindi kwa asilimia 4.0 na samaki wabichi kwa asilimia 2.1.

Pia ametaja ndizi za kupika kwa asilimia 9.4, mbogamboga kwa asilimia 2.1, viazi mviringo kwa asilimia 3.8 , maharage kwa asilimia 3.3 na muhogo kwa asilimia 5.2

Amesema, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka kwa fahalisi za bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 3.2 na petrol kwa asilimia 5.8.

Hata hivyo Kwesigabo ameeleza,  kuhusu uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 63 na senti 35 mwezi Mei, 2015 kutoka mwezi Septemba mwaka huu.

error: Content is protected !!