October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NBC yatumia bilioni 2.5 kudhamini ligi kuu

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imeingia mkataba na Benki ya NBC wenye thamani ya Sh.2.5 bilioni bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkataba huo wa miaka mitatu umesainiwa leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021. Kila mwaka NBC itatoa Sh.2.5 bilioni.

TFF na NBC wameingia mkataba huo wakati tayari ligi kuu msimu wa 2021/22, yenye timu 16 imekwisha kuanza kwa michezo raundi ya kwanza na pili kupigwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi amesema, uamuzi wa kuamua kuwekeza katika mchezo wa mpira wa miguu kwa manufaa ya Taifa na “usitawi wa benki yetu” umetokana na ubora wa ligi hiyo.

“Tumefanya utafiti wa kutosha na kujidhihirisha, uimara wa uendeshwaji wa ligi na hivyo imekuwa rahisi zaidi kufanya uamuzi huu wa uwekezaji,” amesema Sabi

Sabi amesema, NBC imedhamilia kuwekeza kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kwa mwaka 2021/22 imetoa Sh.2.5 bilioni “tukiamini, itaendeleza chachu ya mchezo wa soka Tanzania.”

error: Content is protected !!