Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Biashara NBC yaja na mikopo ya matrekta, zana za kilimo kwa wakulima
Biashara

NBC yaja na mikopo ya matrekta, zana za kilimo kwa wakulima

Mkurugenzi wa Biashara kutoka Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa tatu kulia) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETC Agro Tractors & Implements Ltd, Praveen Chandra (wa pili kulia) kwa pamoja wakionesha mikataba waliyosaini jana jijini Dar es Salaam kutekeleza mpango wa kuwakopesha wakulima matrekta na zana mbalimbali za kilimo. Kulia ni Meneja wa masuala ya Utawala wa kampuni hiyo, Mussa Daudi wakati kushoto ni maofisa wa Benki hiyo ya NBC waliohudhuria hafla hiyo.
Spread the love

KATIKA kuiwezesha sekta ya kilimo kupiga hatua nchini Benki ya Taifa ya Biashara imesaini mkataba na Kampuni ya usambazaji wa zana za kilimo – ETC Agro Tractors & Implements Ltd wenye lengo la kuwakopesha wakulima matrekta pamoja na zana nyingine za kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo jijini Dar es salaam jana, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru amesema lengo la mkataba ni kuongeza tija kwa wakulima hasa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.

Mkurugenzi wa Biashara kutoka Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETC Agro Tractors & Implements Ltd, Praveen Chandra (katikati) kwa pamoja wakisaini mikataba yenye lengo la kutekeleza mpango wa kuwakopesha wakulima matrekta na zana mbalimbali za kilimo. Kulia ni Meneja wa masuala ya Utawala wa kampuni hiyo, Mussa Daudi wakati aliyesimama kushuhudia makubaliano hayo ni Mwanasheria wa Benki hiyo ya NBC.

Amesema NBC kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo katika uchumi wa Tanzania hasa ikizingatiwa inachangia asilimia 30 ya pato la Taifa na kuajiri asilimia 70 ya wafanyakazi wote Tanzania, imeamua kutoa mikopo ya zana hizo kwa wakulima.

“Kwa kutambua hilo tukaona haja kubwa ya kuongeza tija kwa wakulima wetu hawa, kwa hiyo mkataba huu umelenga kuwasaidia wakulima kuongeza matrekta na zana za kilimo ambazo zitaenda kubadilisha kabisa namna wanavyofanya kazi katika kilimo chao,” amesema.

Mkurugenzi wa Biashara kutoka Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETC Agro Tractors & Implements Ltd, Praveen Chandra (katikati) kwa pamoja wakionesha na kubadilishana mikataba ya makubaliano kuhusu mpango maalumu wa kuwakopesha

Amesema huduma hiyo ya mikopo ya zana za kilimo inatarajiwa kuanza Januari mwaka 2022.

“Matarajio yetu ni kwamba itakuwa ni mkopo ambao una riba nafuu, mkopo ambao una masharti nafuu kwa ujumla.

“Kwa mfano hakutakuwa na dhamana nyingine yoyote. Dhamana pekee itakayotumika ni trekta lenyewe au chombo chenyewe lakini mkulima atachanmgia asilimia 25 ya trekta au chombo hicho husika,” amesema.

Amesema pia NBC itaangalia mtiririko wa mauzo ya mkulima husika iwapo anaweza kulipa rejesho la mkopo huo au lah.

“Kikubwa zaidi marejesho ya mkopo huo yatategemea pia kalenda ya kilimo husika, kwa hiyo kama mtu anafanya kilimo cha mahindi ambalo ni zao la msimu, marejesho yatakuwa wakati wa mavuno.

“Kipindi ambacho mkulima hana mavuno labda anafanya matayarisho ya shamba, mkulima hana haja ya kufanya marejesho, tumefanya hivyo makusudi ili kuwawezesha wakulima kulipa mikopo yao bila kuwa na changamoto yoyote,” amesema.

Ameongeza kuwa wakulima wanaweza kwenda kupata mikopo hiyo katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo nchini.

Aidha, akizungumzia mkataba huo kwa niaba ya Meneja Mkuu wa ETC Agro Tractors & Implements Ltd, Praveen Chandra, Meneja wa masuala ya Utawala wa kampuni hiyo Mussa Daudi alisema wakulima watakaopata mikopo hiyo ni wale wenye uwezo wa kulima hekari 15 na kuendelea.

Amesema suala la msingi ni kuhakiki na kujiridhisha iwapo mkopaji ni mkulima kweli.

Aidha, amesema, matrekta hayo pamoja na zana nyingine za kilimo zitakopeshwa kwa wakulima kila mkoa kupitia kwa timu ya watalaam 40 wa kampuni hiyo waliosambaa mikoani.

Pamoja na mambo mengine amesema kampuni hiyo ambayo pia hukodisha matrekta kwa wakulima kupitia program za simu, pia huwa inatoa mafunzo kwa wakulima kabla ya kuwapatia.

“Mara nyingi tumekuwa tukitoa mafunzo ya awali kabla ya kuwapatia matrekta ambapo huwapatia mafunzo haya bure kwa siku tatu,” amesema.

Amesema matrekta ya kampuni hiyo yanauwezo wa kulima hekari zaidi ya 50 bila kutokea hitilafu yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Makongo

Spread the love  MABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet imefika...

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Biashara

Shinda mpaka 1,250,000/= ukicheza shindano la Expanse Kasino

Spread the love  KUBWA zaidi kutoka Meridianbet ni promosheni ya Expanse ambayo...

error: Content is protected !!