Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Biashara NBC yaendelea kutoa zawadi kwa washindi ‘Vuna zaidi na NBC shambani’,
BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaendelea kutoa zawadi kwa washindi ‘Vuna zaidi na NBC shambani’,

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Abdallah Mohamed Malela (wa pili kushoto) akijaribu ubora wa trekta lililotolewa na Benki ya NBC kwa mshindi wa droo ya sita ya kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ ambae ni Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU). Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dastan Kyobya (wa sita kushoto), Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Waziri Barnabas, viongozi waandamizi wa benki hiyo, wakulima na viongozi wa MAMCU.
Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli, pikipiki, guta na trekta kwa washindi wa droo ya sita ya   kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Pia serikali imebainisha kuwa zawadi hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea kasi ya uzalishaji wa mazao ya korosho na mazao mengine katika mikoa hiyo.

Wanachama Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU) pamoja na uongozi wa chama hicho wakifurahia baada ya kukabidhiwa trekta lililotolewa na Benki ya NBC baada ya chama hicho kuibuka mshindi wa droo ya sita ya kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC wakati wa hafla fupi ya kukabidhi ya zawadi hizo iliyofanyika katikati ya wiki mkoani Mtwara.

Zawadi hizo zimegawiwa katikati ya wiki mkoani Mtwara kwa washindi mbambali wa droo hiyo ikiwemo zawadi kubwa ya trekta kwa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi (MAMCU).

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Abdallah Mohamed Malela alisema zawadi hizo zimekuja wakati muafaka kwa kuwa mkoa huo upo kwenye utekelezaji wa mkakati wake wa kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kutoka tani 280,000 zinazozalishwa sasa hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

“Zaidi pongezi nizielekeze kwa MAMCU kwa kuwa wanapokea zawadi hii ya trekta ikiwa ni hivi karibuni tu kama mkoa tuliweka azimio la msingi kwamba kuanzia msimu ujao wa kilimo kila chama kikuu cha ushirika lazima kiwe na shamba darasa lenye ukubwa wa ekari 1500 ili kufikia malengo ya uzalishaji wa mazao ya korosho na mazao mengine ya kimkakati. Kupitia zawadi hii ni wazi NBC imewashika mkono naomba na nyinyi pia muishike mkono,’ alisema.

Malela aliwasisitiza wakulima mkoani humo kuhakikisha wanahifadhi fedha zao benki sambamba na kuongeza nidhamu ya matumizi ya fedha zao hata pale wanapozihifadhi kwenye taasisi za kifedha na wazitumie kwenye mahitaji ya msingi ikiwemo kuwekeza zaidi kwenye zana za kilimo cha kisasa ili kuboresha hali za maisha yao na familia zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dastan Kyobya aliahidi kutoa eneo la ekari 1500 kwa MAMCU ili limike katika kufanikisha shughuli za kilimo cha ushirika huo, ikiwa ni ishara pia ya kuunga mkono nia njema ya benki ya NBC katika kuwasaidia wakulima hao.

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Abdallah Mohamed Malela (katikati) akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi ya zawadi hizo iliyofanyika katikati ya wiki mkoani Mtwara. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dastan Kyobya, Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Waziri Barnabas, viongozi waandamizi wa benki hiyo, wakulima na viongozi wa MAMCU

“Kwa kuwa NBC tayari wameanza kwa kuwazawadia zana za kilimo ikiwemo trekta na sisi serikali ya mkoa tunawapatia eneo la kutosha ekari 1500 ili muweze kufanikia azimo la kulima ekari 1500 katika msimu ujao wa kilimo…hongereni sana’’ alisema Bw Kyobya huku akiiomba benki hiyo kuendelea kufungua matawi mkoani humo sambamba na kuangalia uwezekano wa kutumia wakulima wenye sifa kufungua huduma za uwakala wa huduma za kibenki katika maeneo ambayo benki hiyo haina matawi yake.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Waziri Barnabas alisema tangu kuanza kwa kampeni hiyo tayari jumla ya washindi 139 wamejipatia zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa mikorosho, guta (Toyo) pamoja na zawadi za nyingine ikiwemo kanga, mabegi ya shule na madaftari vikiwa na thamani ya takribani sh milioni 200.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Raymond Urassa alisema kupitia droo hiyo benki ilitoa zawadi za aina mbalimbali zipatazo 26 ikiwemo trekta 1, pikipiki 7, baiskeli 9, pampu za kupulizia dawa mikorosho 8, guta (Toyo)1, pamoja na zawadi za nyingine ikiwemo kanga, mabegi ya shule na madaftari kwa wakulima mmoja mmoja, AMCOS na vyama vikuu ushirika katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

“Naendelea kuwahamasisha wakulima waendelee kupitishia fedha zao kupitia benki akaunti ya NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata,’’ alisema Urassa

Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Bw Waziri Barnabas akizungumza kwenye hafla hiyo.

Kwa upande wao washindi wa droo hiyo waliishukuru benki ya NBC kwa kuandaa kwa kampeni hiyo kwa kuwa imekuwa na msaada mkubwa kwao.

“Zawadi hii ya trekta imekujwa wakati muafaka sana kwa kuwa kwasasa tumeshaanza utekelekezaji wa azimio la kulima ekari 1500 kwa ajili ya kilimo cha korosho na mazao mengine. Tunawashukuru sana NBC kwa kuwa trekta hili litakuwa msaada mkubwa sana kufanikisha hilo. Katika kurejesha shukrani zetu kwao tunaahidi kuendelea kupitisha fedha zetu kupitia akaunti za NBC Shambani ili tuweze kuwania zawadi zaidi,’’ alisema Biadia Matipa ambae ni Kaimu Meneja Mkuu wa MAMCU.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Habari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Dar, Majaliwa azitaka Serikali za Mitaa, Taasisi zijifunze kwao

Spread the loveBENKI ya NMB imewafuturisha wateja wake walio kwenye Mfungo wa...

error: Content is protected !!