Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NBC wasisitiza kukuza michezo, sanaa na utamaduni
Habari Mchanganyiko

NBC wasisitiza kukuza michezo, sanaa na utamaduni

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu adhma yake ya kukuza na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo inayokua kwa kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi katika hafla ya kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza na wageni waalikwa wakati hafla hiyo.

Alisema sekta ya michezo, sanaa na utamaduni ina mchango muhimu katika suala zima la ajira pamoja na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla.

“Pamoja na kuitikia wito wa serikali katika kuinua sekta hii muhimu, benki ya NBC tumebaini kwamba sekta hii ni eneo la kimkakati kiuchumi iwapo sisi kama wadau muhimu tutaiunga mkono,’’ alisema Sabi kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali  wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa.

Sabi alibainisha kuwa benki hiyo ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na wadau wa sekta michezo, sanaa na utamaduni na dhamira hiyo inapimwa kwa namna ambavyo taasisi hiyo hiyo inadhamini matukio mbalimbali ya kimichezo hapa nchini ikiwemo Ligi Kuu  ya Tanzania Bara (NBC Premier League), NBC Dodoma Marathon, mashindano mbalimbali ya mchezo wa golf pamoja na kuunga mkono jitihada za ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo ujenzi wa viwanja vya mpira katika maeneo mbalimbali nchini.

“Hivyo basi kwetu NBC milango ipo wazi wa wadau mbalimbali wa sekta ya michezo, sanaa na burudani ili tuweze kushirikiana katika kukuza sekta hii muhimu lengo likiwa ni kukuza ajira ambayo ni nyenzo muhimu kiuchumi na ustawi wa sekta ya fedha nchini,’’ alisema.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya michezo, sanaa na utamaduni nchini wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza. fla hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano na benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Pamoja na kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola hafla hiyo pia ilihusisha makabidhiano ya taarifa ya namna bora ya kusimamia HAKIMILIKI na ugawaji wa Mirabaha kwa wamiliki wa kazi za sanaa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!