January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NBAA yajiimarisha katika TEHAMA

BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Isaya Jairo

Spread the love

BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), imeunda mikakati kazi itakayodumu kwa miaka mitano hususani katika masuala ya utumiaji wa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na utunzi wa mitihani ya hesabu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi hiyo nchini, Isaya Jairo, amesema, bodi imepanga mikakati kazi mipya itakayowasaidi wanafunzi na waalimu hasa katika masuala yote yanayohusu hesabu.

Amesema, lengo la mkutano huo ni kupata maboresho na maoni tofauti kuhusiana na mikakati hiyo ambayo bodi imepanga.

Jairo ameongeza kuwa, NBAA imepewa jukumu na serikali la kusimamia hesabu Tanzania, hivyo ni lazima ikusanye maoni kutoka kwa wadau tofauti wakiwamo na wanafunzi na walimu, ili bodi ijue changamoto zao na kuangalia jinsi ya kutatua.

Amefafanua kuwa, mikakati hiyo ambayo bodi imepanga itaanza kutumika Julai mosi mwaka huu, ambapo kila Mtanzania ataijua na mwanafunzi atapaswa kuifuata ili kuongeza weledi katika hesabu.

“Tumepata eneo kubwa maeneo ya Bunju, ambapo tumejenga ofisi mpya za TEHAMA, hivyo shughuli zote zitahamia kule na itaaza kutumika tarehe 30 Julai mwaka huu,” amesema.

error: Content is protected !!