April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nassari ‘ashambuliwa’ kwa risasi

Joshua Nassari, Mbunge wa Arumeru Mashariki. Picha ndogo maganda ya risasi zilizotumika kufanya katika shambulio hilo

Spread the love

MAKUMI ya watu wenye silaha, jana usiku wakiwa na bunduki na risasi za moto, walivamia nyumbani kwa mbunge wa Chadema katika jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, kwa lengo la kufanya mauaji, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka mjini Arusha zinasema, watu hao wenye silaha, walivamia nyumbani kwa mbunge huyo, maeneo ya Usa River, majira ya saa tano na nusu usiku wa kuamkia leo Jumamosi.

Kwa mujibu wa Nassari, wakati “watu hao wasiojulikana” walivamia nyumbani kwake, muda mfupi baada ya yeye kurejea kutoka chuo cha MSTCDC (Danish), ambako alikwenda kuhudhuria mafunzo ya uongozi kwa vijana.

“Hawa watu wameruka uzio wa nyumba yangu na kuingia ndani. Walipoingia ndani, walikutana na mbwa na wakaamua kumfyatua risasi kadhaa na kumuua,” ameeleza mbunge huyo mahiri wa Arumeru Mashariki.

Anasema, baada ya watu hao kuingia ndani na kuanza kufyatua risasi, yeye na mkewe walifanikiwa kutoroka kupitia mlango wa uani, kabla ya kuripoti tukio hilo kituo cha Polisi.

error: Content is protected !!