February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NASA wajiondoa kwenye uchaguzi Kenya

Raila Odinga, aliyekuwa mgombea wa Muungano wa NASA

Spread the love

MUUNGANO wa vyama vya Nasa umetangaza kujitoa rasmi katika uchaguzi mkuu wa Kenya uliopangwa kufanyika tarehe 26 Oktoba mwaka huu, anaandika Mwandishi Wetu.

Uamuzi wa kujiondoa katika uchaguzi huo umetangazwa leo na Raila Odinga, mgombea urais wa muu ngano wa Nasa, kwa madai kuwa uchaguzi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu si halali.

Odinga amekishutumu chama cha Jubilee na Rais Uhuru Kenyatta kwa kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi katika kipindi hiki amvbacho kampeni zinaendelea na kusema kuwa hatua hiyo inalenga kukibeba chama hicho katika utangazaji wa matokeo.

Wakati hayo yakiendelea, Rais Kenyatta ameendelea na mikutano yake ya kampeni katika kaunti ya Voi ambapo amewataka Wakenya wasiyumbishwe na Odinga na chama chake na badala yake waendelee kujiandaa na uchaguzi mkuu, Oktoba 26 mwaka huu.

error: Content is protected !!