February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nape Nnauye apata ajali leo asubuhi Liwale

Spread the love

NAPE Nnauye, Mbunge wa jimbo la Mtama,  amepata ajali asubuhi ya  leo tarehe 24 Septemba 2018  akiwa safarini kuelekea wilaya ya Liwale mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Nape pamoja na wengine waliokuwemo ndani ya gari hawajapata madhara makubwa ya kiafya.

Nape alikuwa njiani akielekea Liwale kwa ajili ya kushiriki ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally. Vile vile, alitarajiwa kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya Siasa ya Mkoa wa Lindi.

Hali ya Mbunge huyo, inaendelea vizuri na ameandika katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter, akimshukuru Mungu pamoja  na wanakijiji cha Kibutuka kwa msaada wao wa baada ya kupata ajali hiyo.

Nape aliandika: “Mwenyezi Mungu kaniokoa na ajali mbaya leo asubuhi, wakati natoka Mtama kuelekea kwenye kikao cha chama Liwale. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu. Nawashukuru sana wananchi wa kijiji cha Kibutuka, wamenisaidia sana, Upendo wenu umenigusa sana! Familia,Viongozi na marafiki nawashukuru sana!

error: Content is protected !!