Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NAPE: MSINITIE MAJARIBUNI
Habari MchanganyikoTangulizi

NAPE: MSINITIE MAJARIBUNI

Spread the love

WAZIRI wa Habari Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amewaonya wanahabari wanaokiuka Sheria zilizopo katika utendaji kazi wao. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea).

Nape ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Mei, 2022  jijini Arusha katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.

Nape amesema pamoja na kwamba Serikali ipo kwenye mchakato wa kupitia Sheria kandamizi katika tasnia hiyo lakini bado Sheria hizo zinatumika.

“Katika tasnia ya habari tuliamua kukubaliana katika kipindi hiki cha mpito wakati tunapitia sera sheria na kanuni mbalimbali tutumie busara zaidi ndio maana tupo hapa.

“Ningependa kuwakumbusha wanahabari matumizi ya busara tunayotumia haina maana sheria hazipo zimefutwa, maneno magumu kidogo lakini naomba niyaseme…tunatumia busara ili mambo yaende, hivyo ni busara kujiepusha kuchokonoa uvumilivu wa busara tunayotumia.

“Twendeni salama na nataka niwaombe mbele ya mwajiri wangu msinitie majaribuni nisaidie tupite kipindi cha mpito salama vinginevyo tutakuja kulaumiana sheria zipo hata kama mnazipigia kelele,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema mapitio ya sheria yanayofanyika yamelenga kuboresha zaidi tasnia ya habari nchini.

Waziri huyo amesema mapitio hayo yatazingatia misingi mikuu ya sheria hiyo ambayo ililenga kuifanya tasnia ya habari kuwa taaluma inayojitegemea na kuheshimika.

“Hivyo pamoja na mambo mengine kama taaluma itasaidia katika kuboresha maslahi ya wanahabari na kwa maana ya ajira zao na mapato yao,” amesema Nape.

Amesema lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha inajenga mfumo wa wanahabari kujisimamia wenyewe kwa mujibu wa taaluma kama ilivyo kwa taaluma zingine za sheria na madaktari.

Aidha, amesema inalenga kuhakiisha kila mwanataaluma anawajibika kwa makosa yake mwenyewe badala ya chombo kizima cha habari kuwajibika kwa makosa ya mwanahabari mmoja.

Amesema msingi mwingine mkuu ni umuhimu wa elimu kwa wanahabari ili kuongeza weledi katika kuelimisha jamii nchi na bara zima.

Nape amesisitiza wakati wa kufanya marekebisho watazingatia misingi ya sheria hizo na malengo yake makuu bila kuathiri umuhimu wa kuwa na namna bora ya kutekeleza misingi hiyo na sheria iliyopo.

Aidha, amesisitiza katika kutekeleza jambo hilo watahakikisha maoni ya wadau yanazingatiwa ili kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

error: Content is protected !!