NAPE Nnauye, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la Miss Tanzania 2016 katika Hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam, anaandika Eunice Laurian.
Uzinduzi huo utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo wabunifu wa mavazi, mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania na wakurungenzi wa kampuni mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Hashim Lundega, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency amesema, uzinduzi huo utakuwa wa aina yake na kwamba, burudani kadhaa zitakuwepo.
“Mara tu baada ya uzinduzi huu katika Jiji la Dar es S alaam utahamia Mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi,” amesema Lundega
More Stories
Yanga yapigwa tatu na Simba, yashushwa kileleni
Mshambuliaji Dodoma jiji ashinda tuzo
Katwila awabwaga Makata, Simkoko tuzo VPL