March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nape bado ang’ang’ana na korosho, ahoji 400 mil za wakulima

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama, akichangia hoja bungeni. Picha ndogo zao la korosho lililoibua mjadala bungeni

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amehoji mpango mbadala wa serikali katika kufidia fedha zinazochangwa na wakulima wa korosho, kwa ajili ya kuboresha elimu jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). 

Nape amehoji hayo leo tarehe 12 Novemba 2018 Bungeni jijini Dodoma, akisema kuwa, wakulima wa korosho walipanga kukata kiasi cha Sh. 30 kwa kila kilo ya zao hilo, kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa elimu, lakini kwa hali ilivyo amesema ni vigumu fedha hizo kupatikana.

Nape ameeleza kuwa, katika jimbo lake, wananchi walichanga Sh. 400 milioni kwa ajili ya kuboresha elimu, lakini suala hilo limesimama kutokana na ugumu wa kuzipata fedha hizo.

“ Jitihada za mkoa wa Lindi katika kuboresha elimu, tulipitisha katika kilo moja ya korosho tukate sh. 30 kuboresha elimu, zilichangwa mil. 400 katika jimbo langu, nini mpango wa serikali kuboresha hili suala na kwa hali ilivyo ni vigumu kuzipata hizo fedha, suala hili limesimama,” amehoji Nape.

Akijibu swali la Nape, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Josephat Kandege amewataka wananchi kuwa na subira kwa kuwa serikali itahakikisha suala la kila halmashauri kupelekewa fedha za maendeleo ya elimu linatekelezwa.

error: Content is protected !!