Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nape awapigania walimu bungeni, ataka tume iundwe
Habari za Siasa

Nape awapigania walimu bungeni, ataka tume iundwe

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

MBUNGE wa Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, ameitaka Serikali ya Tanzania, iunde tume maalum ya kuchunguza madai na stahiki zote za walimu nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Nape amesema hayo leo Ijumaa tarehe 23 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yam waka 2021/22.

“Chama Cha Mapinduzi ni chama cha wakulima na wafanyakazi, serikali ya chama cha mapinduzi ni muhimu sana ikashughulika na wafanyakazi wa nchi hii kama mtaji,” amesema Nape.

Amesema, walimu ni karibu asilimia 70 ya watumishi wa umma Tanzania na “tumewakabidhi watoto wetu, vijana wetu na kulifundisha taifa letu, lakini ni bahati mbaya, wizara ya utumishi, hazina na baadhi ya wizara, zimekuwa zikitoa nyaraka na kwa bahati mbaya, zimekuwa hazilitendei haki kundi hili.”

“Nyaraka hizi na taratibu, zimezaa makundi. Kundi la walimu ambao wamepandishwa lakini mpaka wanastaafu hawakupandishwa stahiki zao na kwa sababu hiyo, mafao yao yameharibika baada ya kustaafu,” amesema.

Leah Ulaya, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

Nape amesema, wapo walimu “waliopandishwa kwa barua lakini hawakupandishwa mishahara yao lakini walikutwa na barua zingine za kupandishwa.”

“Kuna kundi la walimu walipandishwa kwa makaratasi, lakini mpaka sasa wamebaki bila nyongeza ya mishahara.”

“Wengine ni walimu ambao walipandishwa kwa barua na hii nafikiri tangu mwaka 2013, baada ya muda ukaandikwa waraka wa kufutwa kwa barua hizo na mimi nafikiri serikali iliona kuna deni kubwa,” amesema Nape

Akiendelea kuchangia, Nape amesema “haya madeni na stahiki zao ni haki zao si hisani na hili jambo si sawa na hatulitendei haki kundi hili. Nyaraka tunazoziandika, zisigeuke kichaka cha kuumiza haki zao na haki huinua taifa.”

“Serikali iunde tume maalumu iende ikachunguze ili hawa walioathirika walipwe na mimi ni matumaini yangu, wizara imepewa vijana, wadogo zangu, watalifanyia kazi hili,” amesema

Waziri wa wizara hiyo ni; Mohamed Mchengerwa na naibu wake ni; Deogratius Ndejembi.

Nape amesema, “jana nimemsikia Rais (Samia Suluhu Hassan), akizungumzia haki, jambo hili ni haki na nataka kuiomba serikali ya chama cha mapinduzi, chama cha wakulima na wafanyakazi, twendeni tukatende haki kwa hawa ambao wamewaacha wananung’unika na hawa wamesimamia uchaguzi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!