December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape aungama kwa JPM

Spread the love

NAPE Nnauye, Mbunge wa Mtama, leo tarehe 10 Agosti 2019 amekwenda kuungama kwa Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Mbunge huyo kijana, amechukua hatua hiyo siku sita baada ya January Makamba (Bumbuli) na Willium Njeleja (Sengerema) kwenda kumwomba radhi kwa kile kilichoelezwa na Rais Magufuli ‘kumtukana’.

Nape amekwenda kumtembelea Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kumwomba radhi kutokana na kuvuja kwa sauti za mazungumzo kati yake na Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu dhidi ya Rais Magufuli.

Mwanasia huyo ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, ameamuo kuomba radhi Rais Magufuli ili kulinda husiano wao na kueleza, anamheshimu kama baba yake na kiongizi wa nchi na chama chake.

“Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini ni mwenykiti wa chama changu na rais wangu. Sababu wote wanajua mambo yaliyopita, yametokea mengi katikati na mimi kama mtoto wa CCM mwanaye nimekosea, ni vizuri niongee na baba yangu.

“…ameniambia amenisamehe, amenishauri namshukuru sana kwa kunisamehe na lakini pili kunielekeza namna ya kufanya ninakokwenda.”

Rais Magufuli amesema, amemsamehe ingawa ilikua mgumu kuchukua hatua hiyo akisema, Nape alimsumbua akimtaka amsamehe ikiwemo kwa kumtumia ujumbe mfupi wa simu usiku wa manane pia kupitia Mama Maria Nyerere.

“Na mimi nimemsamehe kwa dhati, sisi tumeumbwa kusamehe ingawa kusamehe kunaumiza, lakini nimemsamehe,” amesema Rais Magufuli.

Tazama video kamili hapo chini

error: Content is protected !!