January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape atumbua BMT, Malinzi amteua Kiganja

Spread the love

NAPE Nnauye, ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henry Lihaya kwa kutowajibika ipasavyo katika usimamizi wa sera za michezo nchini, anaandika Happyness Lidwino.

Muda mchache baada ya Nnauye kutengua, uteuzi wa Lihaya, Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi amemtangaza Said Kiganja kuwa Kaimu Katibu Mtendaji mpya katika baraza hilo ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Lihaya.

Kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwa ni Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) tangu mwaka 2015.

Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo, amesema amelazimika kumuondoa mtendaji huyo kutokana na kutowajibika katika kupitia sheria ambazo hazina manufaa kwa sekta ya michezo.

“Tunafanya mabadiliko katika baraza hili kwani baraza hili ni moyo wa michezo, kama hatutakuwa na mipango hatutaweza kuendelea katika michezo,” amesema Nnauye.

Waziri huyo amesema ili Tanzania ipige hatua katika sekta hiyo ni lazima kuwe na maaumuzi magumu ili kuweza kusonga mbele nakufikia malengo yaliyokusudiwa .

Nnauye amesema Kiganja ataanza kazi iliyomshinda Lihaya ya kubadilisha vifungu vya sheria ambazo zimepitwa na wakati na kuwa na katiba hizo ili tuweze kusonga mbele katika sekta ya michezo.

error: Content is protected !!