August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape atuma salamu za rambirambi

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

Spread the love

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa pamoja na wanamichezo wote kufuatia kifo cha mchezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Mbao FC, Ismail Mrisho Khalfani kilichotokea jana katika michuano ya kombe la vijana, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Nape pamoja na watendaji wengine wa wizara wamepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mchezaji huo wakati timu yake ilipokuwa ikicheza na Mwadui FC katika uwanja wa Kaitaba, Kagera kwani ni pigo katika tasnia ya michezo nchini hasa vijana.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji, Ismail Mrisho Khalfani. Kifo chake ni pigo kwa tasnia ya michezo hususani vijana ambao ndio tegemeo la taifa letu, nimehuzunishwa sana kwa sababu kabla ya mauti kumkuta aliweka kuipatia timu yake bao la kwanza lililopelekea ushindi wa goli 2-0,” amesema Nape.

Kufuatia kifo hicho, mwili wa Ismail unatarajia kusafirishwa leo kutoka mkoani Kagera kwenda nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya taratibu zingine za mazishi ambayo pia yanatarajiwa kufanyika leo jioni jijini Mwanza.

Aidha Waziri Nape ametuma pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na wapenzi wa klabu ya Yanga kufuatia kifo cha mzee Yusuph Mzimba kilichotokea Desemba 3 mwaka huu na ameiomba jamii yote ya wapenda michezo kuwa na uvumilivu na watulivu wakati wote wa msiba.

error: Content is protected !!