Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari Nape atangaza neema kwa vyombo vya habari, waandishi
Habari

Nape atangaza neema kwa vyombo vya habari, waandishi

Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania, Nape Nnauye ameagiza taasisi za Serikali zilizokuwa zinasita kutoa matangazo kwa vyombo vya habari binafsi kuacha na kutoa kwa usawa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Aidha, ametangaza mwaka mmoja zaidi kwa waandishi wa habari wasiokuwa na elimu ya diploma ili kuruhusu majadiliano baina ya Serikali na wadau wa habari kuhusu Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari yam waka 2016.

Sheria hiyo inaeleza, mwandishi wa habari ili aweze kutambulika anapaswa kuwa na elimu ngazi ya diploma. Utekelezaji wake ulipaswa kuanza tarehe 1 Januari 2022, baada ya kipindi cha mpito cha miaka mitano cha waliokuwa hawana elimu hiyo kwenda kusoma kumalizika.

Waziri Nape amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 10 Februari 2022, katika kikao chake na wahariri mbalimbali kilichofanyikia makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.

“Nimezielekeza taasisi zilizokuwa zinasita kutoa matangazo na kulipa madeni, zitoe matangazo na madeni. Hatuna sababu ya kubaguana, wote mna macho sawa. Tutaangalia utaratibu kama amepewa fulani, kesho apewe mwingine,” amesema Nape

Kuhusu utekeleaji wa sheria hiyo ambayo wakati inatungwa yeye (Nape) ndiye alikuwa waziri amesema, “mimi nikiwa waziri, nilisimamia ile sheria, lakini mazingira ya wakati ule na sasa ni tofauti, mwaka 2016 na 2022 ni tofauti. Hili la elimu tutoe mwaka mmoja ili tuone nini cha kufanya tukikutana kwenye majadiliano.”

Waziri huyo amesema, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha inashirikiana vilivyo na wadau na “tutatumia busara, tutashikamana kwa pamoja na nia ya Serikali ya awamu ya sita ni nzuri. Mimi najua tulikotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko ni ndefu. Tunaomba tuaminiane tutafika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!