August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape amtambulisha mrithi wa Mwambene

Spread the love

NAPE Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amemtambulisha Hassan Abbas, Mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari Malelezo, anaandika Regina Mkonde.

Uteuzi wa Abbas unafuatia uhamisho wa Assah Mwambene, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda ambapo alipangiwa kazi nyingine.

Katika utambulisho wa leo kwa wanahabari, Mkurugenzi huyo mpya amesema; “Mtarajie mabadiliko makubwa kwenye idara, naahidi mabadiliko ya kiutendaji lakini siwezi kuyafanya mabadiliko hayo peke yangu bila ya ninyi wadau wa tasnia hii kunipa ushirikiano.”

Aidha Nape ameviomba vyombo vya habari na wadau wa habari kutoa ushirikiano chanya kwa mkurugenzi huyo atakapokuwa akitekeleza majukumu yake yote kama Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo.

“Mpeni ushirikiano mkurugenzi mpya kwani chombo cha habari lazima kifuate sheria tulizonazo na katika hili niwe muwazi ya kwamba, hakuna uhuru usio na mipaka ingawa mimi kama mwandishi wa habari mwenzenu ninatetea uhuru wa habari na haki ya kupata habari,” amesema.

Uhamisho wa Mwambene aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo ulifanyika tarehe 7 Machi 2016 huku uteuzi wa Hassan Abbas kujaza nafasi hiyo ukianza tarehe 5 Agosti mwaka huu.

 

error: Content is protected !!