Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nape aitabiria mabaya CCM
Habari za SiasaTangulizi

Nape aitabiria mabaya CCM

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama, akichangia hoja bungeni. Picha ndogo zao la korosho lililoibua mjadala bungeni
Spread the love
MBUNGE wa Mtama kwa tiketi ya CCM, Nape Nnauye ameitabiria mabaya chama chake, kuwa kisipokuwa makini kitakufa na kupotea kabisa katika mikoa ya Kusini kama wataendelea kushirikia msimamo wao wa kufuta ushuru katika mauzo ya zao la korosho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Nape akiunga mkono na Mbunge mwenzake, Hawa Ghasia wa jimbo la  Mtwara Vijijini, wamesema hawakubaliani na mapendekezo ya Serikali ya kutaka kufuta ushuru wa asilimia 65 wa fedha zinazotokana na mauzo ya korosho nje na kubainisha kuwa wanachokifanya ni bomu ambalo linaenda kukiua chama chao cha CCM katika mikoa ya Kusini.

Wabunge hao wametoa walitoa kauli hizo walipokuwa wanachangia mjadala wa bajeti ya Serikali, wamesema wapo tayari  kudhalilishwa na wabunge wenzao waliopangwa kuitetea Serikali katika suala hilo la Korosho huku mawaziri wawili wakisimama kutetea jambo hilo.

Tayari baadhi ya wabunge wametishia kufanya maandamano iwapo Serikali haitatoa asilimia 65 za ushuru wa mauzo ya korosho nje kwa ajili ya maendeleo ya zao hilo.

Pia, wanapinga mabadiliko ya Sheria ya Korosho yanayokusudiwa kufanywa na Serikali ili ushuru huo upelekwe katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

Aliyeanza kuzungumza alikuwa Nape aliyebainisha kuwa ukizungumzia korosho unazungumzia maisha ya watu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na mingine inayolima korosho.

“Wakulima wa pamba wakizungumza pamba wanazungmza maisha, sisi hatuna mifugo, almasi na tukizungumza korosho ni maisha na linapozungumzwa hili ushabiki uwekwe pembeni, tunazungumza maisha,” amesema.

“Hili jambo tulilizungumza katika wizara ya Kilimo na mwenyekiti wa Bunge (Mussa Azzan Zungu) ulikuwapo na tulizungumza nje na hatukukubaliana.

Amebainisha kuwa dhana kuwa mapato yote ya korosho yasaidie mikoa ya Kusini si kweli, kwamba yatafanya shughuli nyingine, “badala ya kutuletea fedha unaleta sheria ya kuzifuta kabisa, huku ni kutudharau kwa hali ya juu, mimi nadhani ushauri wangu hebu zungumzieni namna ya kuleta fedha na hii sheria ondoeni kwanza.”

“Dk. Mpango mbona unazungumza na korosho na katani peke yake, mbona nia ovu, unapora fedha halafu unaleta sheria hii, maisha haya ni maisha yetu. Tunaopata madhila mabaya zaidi katika gesi, mbaazi imeanguka.”

Huku akizungumza kwa uchungu Nape amesema, “Wanaosema si hela zetu hiki kiatu hamvai nyinyi tunakivaa sisi. Dk. Mpango kuweni na huruma na mapendekezo haya yanakwenda kuiua CCM Kusini, yanakwenda kutuweka mahali pagumu sana.”

Kauli hiyo ilimuinua Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya akimtaka Nape anapochangia kutowashawishi wananchi wa mikoa ya Kusini kupinga mambo mbalimbali yanayoazimiwa kufanywa na Serikali.

Kwa upande wake Ghasia ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti amesema,” kuna wabunge wamekaa vikao, wameandaliwa waje kutudhalilisha wabunge tunaowatetea wakulima.”

“Wabunge wote tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu, anayetoka katika pamba atetee pamba, anayetoka katika madini atatetea madini yake na anayetoka katika korosho atatetea wa korosho.’

“Niwahakikishia wakulima wanaolima korosho wabunge wao tutapambamba na hata haki isipopatikana ila tutawatetea. Tunaambiwa sisi wabinafsi, korosho inalimwa kwa kiwango kikubwa na mikoa miwili au mitatu lakini tulipokaa katika kamati tukakubaliana na kwenda mikoa 17,”

Amesisitiza, “Leo tunaambiwa sisi wabinafsi, kuna watu wanakuja kusimama wanasema wanaijua korosho kuliko sisi. Mimi utafiti wangu wa shahada ya kwanza na ya pili inahusu korosho. Leo mtu anakuja humu anaijua korosho na ninasema kila mtu atetee lake na wananchi mjiandae kuwasikia.”

Baada ya Ghasia kumaliza kuchangia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisema Serikali haina nia ovu na suala la korosho na haina nia ya kuwanyanyasa wakulima wa zao hilo.

Katika ufafanuzi wake kuhusu mvutano huo, mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema jambo hilo lisiligawe Bunge na kuwataka wabunge kusubiri hoja zitakazotolewa na Serikali wakati ikijibu jambo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!