Tuesday , 18 June 2024
Habari za SiasaTangulizi

Nape abanwa mbavu

Spread the love
VIDEO inayoonesha kina mama wakigombana kwa ajili ya maji, katika kijiji cha Shuka, kata ya Navanga mkoani Lindi, imemtesa Nape Nnauye, mbunge wa jimbo la Mtama. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbunge huyo alianza kujitetea, kwamba uhaba wa maji katika kijiji hicho si mkubwa kwa kiasi kilichoonekana kwenye video hiyo. Hatua hiyo iliwasukuma watu wengi kuanza ‘kumshughulikia.’

Taarifa hiyo, iliripotiwa na chombo cha habari cha Azam na baadaye kuwekwa mtandaoni, jana tarehe 26 Oktoba 2019. Kutokana na muktadha wa video hiyo, iliwasukuma watu wengi kuanza kuchangia na ndipo Nape alipojitokeza.

Niliwaza mwanzo kunyamazia hii habari lakini nadhani haitakuwa sawa maana uongo usipojibiwa unaaminiwa! Mimi ni mkaazi wa kijiji hiki, wiki kadhaa zilizopita nilikuwa hapa, tutafuteni mengine ya kusema badala ya kujifichia kwenye hili si sawa! Huu ni uzushi wa ajabu sana!” aliandika Nape kwenye ukurasa wake wa twitter.

Baada ya jibu hilo la Nape, mtu aliyejitambulisha kwa jina la Martin M. M alimjibu, kwamba kilichomo kwenye video hiyo ni ukweli mtupu na kama si kweli, walioripoti taarifa hiyo awapeleke mahakamani.

“…AzamTv ndio source (chanzo) ya habari hii. Nafikiri ni vyema sasa kuwapeleka mahakamani, lakini zingatia, wananchi wa eneo hilo na kiongozi wao wameeleza, tuwasaidie, tusiwakane,” ameandika Martin M.M.

Katika kujitetea Nape aliandika “hivi hujiulizi kwanini stori (habari) hawakubalance (hawakuuliza) wenye dhamana kama mbunge juu ya hoja hii?Ni kweli kwamba inakuingia akilini kuwa hicho ndio chanzo pekee cha maji kwa kijiji chenye zaidi ya miaka 30?

Saidi Livemba alimjibu Nape, aliandika “Nape wewe mbunge wangu kabisa ila katika hili napingana na wewe. Kijiji cha Shuka kipo kata ya Navanga, umbali kutoka kijiji cha Shuka mpaka makao makuu ya jimbo ni kama km 70 hivi. Mwisho wewe ulikuwa Mtama na sio Shuka.”

Nape akajitokeza tena “kwa taarifa yako sio mara ya kwanza mie naenda kulala Shuka! semeni ya kweli haya sio maji pekee wanayotumia wanaShuka hapana!”

Kwenye mjadala huo Alfaxad Khamis aliandika “kwahiyo ulipokuwa hapo, ukifanya nini? Mkiambiwa ukweli mnang’aka watu wanagombania maji mko bize na ndege, oneni aibu acheni ushamba tatueni kero na changamoto za wananchi, maendeleo ya vitu hayana maana ikiwa wananchi wanapata tabu.

Mgomvi Mshauri 2020 aliandika “Azam wameweka na picha wamama wanapigana na tukayaona maji machafu mnayokunywa, kibali au nawe tuoneshe ukweli siyo hizi porojo za kiwango cha chekechea.”

Mwengine anayejitambulisha kwa jina Mr Ndikwegha aliandika  “leo nakushangaa Nape unabishana na Tv (Televisheni) huku video ikiwepo, dah inasikitisha sana.”

Tangu upate ubatizo mpya sasa hivi ndugu yangu mwendo wa kusifia tuu,” aliandika mtu anayejitambulisha kwa adresi ya FreeErickKabendera.

Fatma Katume, Rais Mstaafu wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), akichangia video hiyo aliandika “video ya wanawake wanagombania maji Lindi imenisumbua sana.

“Miaka 58 baada ya Uhuru na bado wananchi wanaishi vile na Serikali ya Wananchi inanunua madege? Inachukuwa mabilioni inaingiza kwenye uchumi wa mabeberu badala kupeleka maji vijijini?”

Mama mmoja kwenye video hiyo alipohojiwa alisema “wanakijiji wa Shuka hatuna maji, na hata wanaume wetu hatuna nafasi ya kupumzika nao, muda wote sisi tunalala kisimani na muda wote sisi tunahangaika kwa masuala ya maji.”

Mwanakijiji mwingine alimwambia mwandishi kwamba, shida ya maji kwenye kijiji hicho ni kubwa na hata kushindwa kupata maji ya kuoshea maiti.

“Ukiona labda Simba anakuja mnakimbizana, sasa haya ni maisha ya binadamu kukimbizana na Simba? Imefikia hatua maiti ataka kuoshwa lakini maji hamna, yakaenda kuchukuliwa maji ya bahari, kweli maiti aoshwe kwa maji ya bahari?” alihoji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!