July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nani kati ya hawa kupenya?

Spread the love

WAPENZI wa soka duniani leo wanatarajia kushuhudia mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2015 iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC). Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Wanasoka wanaopigania tuzo hiyo ni Yacine Brahimi ambaye ni Raia wa Algeria na mchezaji wa klabu ya FC Porto.

Mchezaji wa pili kati ya watano wanaowania tuzo hiyo ni mchezaji wa timu ya Swansea, Andre Ayew ambaye ni Rais wa Ghana. Yeye aliiwezesha timu ya taifa lake kutinga katika fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezaji wa tatu ni Yaya Toure wa timu ya Manchester City na Ivory Coast, ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora barani mwezi Februari mwaka huu.

Mwingine kwenye kinyang’angiro hicho ni mshambuliaji wa timu za Gabon na Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, nyota huyu amekuwa na bahati ya kuzifumania nyavu mara kwa mara ndani ya mwaka huu.

Sadio Mane ambaye ni Raia wa Senegal ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na kufanya vizuri akiwa na timu ya Southampton mwaka huu. Upigaji kura ulifungwa rasmi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Waliowahi kuchukua tuzo hiyo miaka ipiyopita ni Yacine Brahimi (2014), Yaya Touré (2013), Christopher Katongo (2012), André Ayew (2011), Asamoah Gyan (2010).

error: Content is protected !!