September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nani kampa sumu Mangula? Hakuna jibu

Philiph Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM

Spread the love

NANI aliyempa sumu Mzee Phillip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)? Ni swali ambalo halijapatiwa majibu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limewataka watu kutouliza uliza swali hilo kwa maeleza kwamba “uchunguzi ukimamilika wataelezwa.”

Mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 27 Machi 2020, SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amesema, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Jeshi linapeleleza kesi nyingi, kila tunapokamiliha upelelezi tunapeleka jalada kwa mwanasheria  wa serikali. Sasa sioni kama inafurahisha kila siku kuuliza imefikia wapi?

“Ikikamilika tutawaambia, si kazi yetu kuwaambia kila hatua tunayofikia, tuna kesi nyingi lakini mara nyingi tukikamIlisha tunawaambia kwamba wahusika wanapelekwa mahakamani,” amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza:

“Habari nyingine si habari, kwamba nieleze sasa hivi nimeandika maelezo ya watu wawili, halafu kesho nimepata na kielelezo. Itakuwa ni mambo ya kitoto na hayako katika maadili ya kazi zetu.”

Tarehe 9 Machi 2020, Kamanda Mambosasa alisema, uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, umebaini mwili wa Mzee Mangula ulikuwa na sumu.

Kamanda Mambosasa alisema, uchunguzi wa tukio hilo lililotokea tarehe 28 Februari 2020, unaendelea.

Mzee Mangula aliugua ghafla akiwa katika Ofisi Ndogo za CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam baada ya kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati Kuu ya chama hicho.

error: Content is protected !!