Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nanenane Singida, Dodoma iwe endelevu – Waziri Jafo
Habari za Siasa

Nanenane Singida, Dodoma iwe endelevu – Waziri Jafo

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

SELEMAN Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ametoa maagizo kwa wakuu wa mikoa ya Dodoma na Singida na halmashauri zote kuhakikisha, maonesho ya wakulima nanenane yanakuwa endelevu. Anaandika Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Jafo ametoa maagizo hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya nzuguni Jijini Dodoma tarehe 4 Agosti 2019.

Akifungua maonesho hayo Jafo alisema, maonesho hayo ni kwa lengo la kutoka elimu kwa wakulima, hivyo ni wajibu wa halmashauri zote kuhakikisha zinaendeleza maeneo hayo sambamba na kuwepo kwa afisa kilimo, ambaye atafanya mahali hapo kuwa sehemu ya kituo cha kazi.

“Natoa agizo sasa kuwa, maonesho ya nanenane yawe maonesho endelevu. Kumekuwe na tabia ya kuacha maeneo na kuyatelekeza na kufanya sehemu ya kusubiri ufike msimu mwingine ili muweze kulupana posho.

“Ni lazima kila halmashauri zote kuhakikisha zinaendeleza kilimo katika halmashauri husika na kumteua bwanashamba kukaa katika eneo husika kama sehemu ya kituo chake cha kazi, ili kutoa elimu bora kwa wakulima na wafugaji,” alisema.

Kuhusu utafiti Jafo alisema, ni wakati wa watafiti kuhakikisha wanafanya utafiti kwa mazao yote ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti wa wanyama.

“Katika hali ya utunzaji wa mazingira, sasa natoa maelekezo badilisheni upandaji wa miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira badala ya kupanda miti ya ajabu, pandeni miti ya matunda ili kupunguza tatizo la utapia mlo,” alisema Jafo.

Dk. Binilith Mahenge, Mkoa wa Dodoma alisema, pamoja na kuwepo kwa maonesho hayo, bado kunachangamoto ya kutokuwepo kwa maelewano kati ya TASO na serikali kusimamia shughuli hizo, jambo ambalo linasababisha wadau kushindwa kuwekeza katika maonesho hayo.

Hata hivyo, anewahamasisha Watanzania hususani wakazi wa Dodoma kujiunga katika Bima ya Afya iliyoboreshwa.

Dk. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Singida alisema, nanenane imekuwa mkombozo kwa wakulima wa Singida kwa kuweza kulima kilimo cha kisasa pamoja na kuwa na jiji la nyuki la kitaifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!