Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Nanenane: Mikakati kuiinua Simiyu yawekwa hadharani
Habari Mchanganyiko

Nanenane: Mikakati kuiinua Simiyu yawekwa hadharani

Spread the love

ANTHONY Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ameeleza mikakati ya kupunguza umasikini mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ripoti ya Hali ya Umasikini kwa mwaka 2017/18, iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonesha, Mkoa wa Simiyu unashika nafasi ya pili kwa umasikini ikiwa na kiwango cha asilimia 39, ukitanguliwa na Mkoa wa Rukwa wenye umasikini kiwango cha asilimia 45.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wakulima nchini ‘Nanenane’ yaliyofanyika mkoani humo leo tarehe 8 Agosti 2019, Mtaka amelitaja zao la pamba kuwa ni mkombozi wa wananchi wa mkoa huo katika kujikomboa kiuchumi.

Mtaka amesema mkoa wa Simiyu unazalisha pamba zaidi ya asilimia 55 kwa mwaka na kwamba mwaka huu unatarajia kuzalisha tani kg 160 milioni, hivyo kama serikali itatoa fedha kwa ajili ya uanzishaji viwanda vya uongezaji thamani zao hilo na vya nguo, wakulima watapata soko na kujikwamua kiuchumi.

Ameeleza kuwa, bidhaa zinazotokana na zao la pamba hapa nchini zina soko kubwa na la uhakika, na kwamba kama viwanda vitajengwa kwa wingi vitatoa ajira kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kuinua kipato cha wakulima.

“EPZ kwa wiki wanazalisha pic laki 4 za jinzi, wanaimport fabric ambayo ni sawa na asilimia 70 ya pamba inayozalishwa nchini, tukiwa tunatengeneza kutoka kwenye shamba kufika kwenye hatua ya fabric ‘kitambaa’ soko letu la ndani zaidi ya asilimia 70 ya pamba tuliyonayo tutairudisha ndani,” amesema Mtaka na kuongeza.

“Wanafunzi milioni 12 wakishona suruali,  shati na sketi hakuna nguo ya 5,000 tukipata 10,000 tuna 120 bilioni. Hata tukitafuta muwekezaji angeihitaji tumuhakikishie soko aidha tumpe soko la elimu, jeshi au sekta ya afya, angepata soko la uhakika.

Aidha, Mtaka ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Idara yake ya fedha na utafiti kutoa andiko la upembuzi yakinifu pamoja na mpango wa bishara kuhusu kuwepo kwa viwanda vya nguo mkoani Simiyu.

 “Tumeiomba kurugenzi yao ya fedha na utafiti waje na andiko la mradi lakini andiko la biashara, ili tunapozungumza tunataka kuwekeza kwenye viwanda vya nguo.

“Wizara wana fedha za miradi ya mkakati, tumeoma fedha zilizorudishwa wizarani kutoka kwenye halmashauri zilizoshindwa kuendesha miradi ya kimkakati, tupatiwe ili tuwekeze,” amesema Mtaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!