WACHEZAJI nane kutoka klabu tofauti ndani ya Ligi Kuu nchini England wameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa Ligi hiyo kwenye msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Ligi hiyo ilimalizika wiki mbili zilizopita na klabu ya Manchester City kutwaa taji hilo mara baada ya kuwa na msimu mzuri na wamafanikio chini ya kocha Pep Guardiolla.

Waliongia kwenye kinyang’anyiro hiko ni kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Kelvin De Bruyne, Kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes, mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane na Jack Glealish kutoka Astorn Villa.
Wengine ni Ruben Dias mlinzi wa kati wa kikosi cha Manchester City, mshambuliaji wa timu ya Liverpool Mohammed Salah, Tomas Soucek kutoka Westham na Mason Maount wa klabu ya Chelsea.

Wachezaji hao nane walichaguliwa mara baada ya kuwa na msimu mzuri kwenye klabu zao na wadau na mshindi atachaguliwa kwa kupigiwa kura.
Leave a comment