Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo Nandy azindua Nandy Beauty Product
MichezoTangulizi

Nandy azindua Nandy Beauty Product

Nandy Beuty Product
Spread the love

KATIKA kuhakikisha anaunga juhudi za serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Msanii wa muziki wa kizazi kipya Faustina Mfinanga ‘Nandy’ amezindua rasmi bidhaa zake za mafuta ya kupaka na sabuni za kuogea. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Msani huyo anayetamba kwa sasa na kibao chake cha Ninogeshe, amewaambia waandishi wa habari jijini Mwanza leo kuwa lengo la kuleta bidhaa hizo sokoni ni kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo tangu utotoni.

Nandy ambaye ni kati ya wasanii wanawake wanaofanya vizuri kwa kuimba nyimbo laini zenye mashairi ya kuelimisha, amesema pamoja na kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuwa mfanyabiashara mkubwa pia bidhaa hizo zitachangia kukuza pato la taifa.

Pia alisema kuwa kwa muda mrefu mashabiki wake walikuwa wakimuuliza na kutamani kuona bidhaa zake na kwamba sasa amekata kiu yao kwa kuleta bidhaa hizo bora aina ya Nandy Beuty Soap na Nandy beuty Jelly zenye manukato mazuri.

Nandy ambaye alianza kuchomoza kwenye muziki wa kizazi kipya mwaka 2016, amesema kuingiza sokoni bidhaa zake itasaidia pia kuongeza ajira kwa vijana huku akiwaomba mashabiki zake kusapoti kwa kununua bidhaa hizo.

“Bidhaa hizi za mafuta ya kupaka na sabuni siyo kwa wanawake pekee ni kwa ajili watu wote na kwa lika zote na bidhaa hizi zinapatikana kote nchini,” alisema Nandy.

Mkurugenzi wa kampuni ya Grace Product, Pastasesa Kasisi, ambao ndiyo watengenezaji wa bidhaa hizo, alisema msanii huyo aliwafuata na kuwaeleza juu ya ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa jambo ambalo waliamua kuungana na kutengeneza bidhaa hizo.

Kasisi amesema bidhaa hizo zinazotengenezwa na kampuni yao ni za asili na hazina madhara kwa watumiaji kwani zimetengenezwa na mimea ambayo ni mizuri kwa kiwango cha kimataifa.

Mmoja wa wasambazaji maarufu Kanda ya Ziwa wa bidhaa za Grace Product, Mayalla Zakaria amesema bidhaa hizo zitakuwa zinapatikana katika maduka yote ya jumla na rejareja katika mikoa yote huku akidai bei ya bidhaa hizo ni za kawaida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

error: Content is protected !!