
Kikosi cha timu ya Namungo wakati wakiondoka nchini Tanzania
KIKOSI cha wachezaji wa Namungo pamoja na viongozi kimeondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Namungo imeondoka jana majira ya saa 3:45 usiku kutoka Uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam kuelekea nchini Morocco wakipitia Doha Qatar.
Mchezo huo wa kwanza wa kundi D, utapigwa tarehe 10 Machi 2021, kwenye mji wa Casablanca.
Namungo ambayo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza imepangwa kwenye kundi D, sambamba na klabu za Raja Casablanca, Pyramid na Nkana Red Devil.
More Stories
Mayele atetema Mwanza, mabao 14 sawa na Mpole
Kim aita 28 Stars
Mauya miwili tena Yanga