May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Namungo kuwakabili Waangola Kombe la Shirikisho

Namungo FC

Spread the love

KLABU ya Soka ya Namungo imepangwa kucheza na CD 1 de Agosto kutoka nchini Angola kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kwenye hatua ya 32 bora mara baada ya kuchezeshwa Droo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea) .

Droo hiyo imechezeshwa leo 8 Januari, 2021 jijini Cairo, Misri ambapo safari hii Namungo itaanzia ugenini nchini Angola kwa mchezo wa kwanza unaotarajia kupigwa tarehe 13 au 13 Febuari 2021.

Namungo inakutana na Costo de Agosto ikiwa ni kwa mara ya kwanza inashiriki michuano baada ya kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kufungwa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba.

Kama Namungo itafanikiwa kuwaondoa waangola hao kwa kupata matokeo kwenye michezo miwili itakuwa imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi.

Namungo ambayo inatokea Luangwa, Lindi imefanikiwa kufika hatua hii ya mzunguko wa tatu ni mara baada ya kuwaondoa Rabita katika hatua ya awali kwa mabao 3-0, na pia ikafanikiwa tena kuwatoa Al Hilal Obed kutoka nchini Sudan kwa mabao 5-3 katika michezo yote miwili.

Costo de Agosto imeingia kwenye michuano hii mara baada ya kuondoshwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika na klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa bao 1-0 kwenye michezo yote miwili.

Timu hiyo ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu nchini Angola kwenye msimu wa 2019/20 kwa tofauti ya pointi tatu na mabingwa wa Ligi hiyo klabu ya Petro De Luanda.

Namungo FC chini ya kocha Hemed Morocco itakuwa inafukuzia kuweka rekodi yao kwa mara ya kwanza barani Afrika kwa kufuzu hatua ya makundi kwa timu ambao inamsimu wa pili kwenye Ligi Kuu.

error: Content is protected !!