December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Namungo kutupa karata ya kwanza leo kimataifa.

Kikosi cha timu ya Namungo FC

Spread the love

 

TIMU ya soka ya Namungo FC leo inashuka uwanjani kuwakabili CD 1 Agosto kutoka Angola kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambapo Namungo FC atakuwa mgeni kwenye mchezo wa kwanza baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuamua michezo yote miwili ichezwe nchini Tanzania.

Namungo wanashuka leo baada ya mchezo uliopangwa kuchezwa awali nchini Angola kufutwa na CAF, kutokana na maafisa wa nchini humo kuishikilia timu ya Namungo FC, wakiwataka wakae karantini au kurejea Tanzania mara baada ya wachezaji wao wawili kukutwa na virusi vya corona.

Tayari CAF ilishatoa muongozo kuhuszu mchezo huo na timu yoyote itakayofuzu hatua inayofuata hatizingatiwa kwenye viwango wakati wa uchezeshwaji wa droo ya makundi itakayofanyika kesho tarehe 22 Februari 2021, jijini Cairo nchini Misri.

Kama Namungo atafanikiwa kupita kwenye hatua hii ataingia moja kwa moja kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza.

error: Content is protected !!