May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Namungo kukamilisha ratiba dhidi ya Pyramids

Kikosi cha timu ya Namungo wakati wakiondoka nchini Tanzania

Spread the love

 

KIKOSI cha Namungo FC leo kitashuka dimbani kwenye mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids kutoka Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Namungo ambayo ipo kwenye kundi D, kwenye michuano hiyo, itashuka dimbani nchini Misri majira ya saa 4 usiku.

Kwenye kundi hilo Namungo inashika nafasi ya mwisho ikiwa haina pointi mara baada ya kukubali kichapo katika michezo yote mitano iliyocheza kwenye hatua hiyo mpaka sasa.

Namungo mpaka sasa amecheza michezo mitano nakupoteza yote huku wakiwa hawajafunga bao hata moja na kuruhusu jumla ya mabao nane mpaka sasa.

Waliofuzu mpaka sasa kwenye kundi hilo ni Raja Casablanca wakiwa na pointi 15, baada ya kucheza michezo mitano ambapo pia nao leo watashuka uwanjani dhidi ya Nkana Red Devil kutoka Zambia.

error: Content is protected !!