Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Namibia yaigomea fidia ya Ujerumani
Kimataifa

Namibia yaigomea fidia ya Ujerumani

Spread the love

RAIS wa Namibia, Hage Geingob amekataa kupokea fidia iliyotolewa na serikali ya Ujerumani, kama fidia ya mauaji ya kimbari. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Serikali ya Ujerumani inapaswa kuilipia fidia Namibia kufuatia mauaji makubwa ya kimbari yaliyofanywa na wanajeshi wake, dhidi ya Wanama na Waherero wa Namibia, kati ya mwaka 1904 na 1908.

Katika tukio hilo, jeshi la Ujerumani liliuwa mamia ya maelfu ya watu wa jamii ya Herero na jamii ya Nama, wakati wa ghasia za kupinga ukoloni.

Taarifa zinasema, asilimia sabini na tano (75%) ya idadi ya watu wa Herero na nusu ya idadi watu wa Nama waliuawa katika kipindi hicho.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja takribani miaka miwili tangu kiongozi wa ujumbe wa Ujerumani katika mazungumzo hayo, Ruprecht Polenz, kunukuliwa akisema, kiasi kinachodaiwa na Namibia ni kikubwa mno, kuliko ambacho taifa hilo linaweza kukitoa.

Hata hivyo, Polenz alisema, serikali ya Ujerumani iko tayari kuongeza msaada wa kimaendeleo kwa Namibia; na kuongeza kiwango kingine ambacho hata hivyo hakikutajwa wazi.

Ujerumani na Namibia zimekuwa zikijadiliana kwa miaka mitatu sasa juu ya fidia hiyo.

Nchi hizo mbili zilianza majadiliano juu ya fidia ya kimbari tangu mwaka 2015 na tayari wamekuwa na mazungumzo mara nane hadi sasa.

Ukurasa wa Twitter wa ofisi ya rais huyo wa Namibia umeweka picha ya rais Geingob na Ngavirue.

Rais Geingob alikuwa anatoa muktasari wa majadiliano kati ya timu ya majadiliano ya serikali ya Namibia na wawakilishi kutoka Zed Ngavirue.

“Fidia iliyotolewa sasa na serikali ya Ujerumani bado haijakubaliwa na serikali ya Namibian,” taarifa kutoka kwa Rais ilieleza. Hakukuwa na maelezo zaidi yaliyotolewa kufafanua uamuzi huo.

Aliongeza: “Ujerumani imekubali kuomba radhi lakini imekataa kufikia maafikiano kati yao ya kuuguza majeraha waliyoyaacha.”

Mwanzoni mwa karne ya 20, wanajeshi wa Ujerumani waliuwa maelfu na maelfu ya Wanama na Waherero wa Namibia, ambayo wakati huo ilijulikana kama Ujerumani ya Kusini Magharibi mwa Afrika. Kuanzia mwaka 2015, Ujerumani imekuwa ikiyatambua rasmi mauaji hayo kuwa ya kimbari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!