Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Naibu Waziri Mavunde awafunda vijana 
Habari Mchanganyiko

Naibu Waziri Mavunde awafunda vijana 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Anthony Mavunde,akizungumza na vijana mbalimbali (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa LAPF mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Konganano la Vijana duniani.
Spread the love

VIJANA nchini wametakiwa kuwa mabalozi waaminifu katika kulinda amani ya nchi, anaandika Dany Tibason

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Anthony Mavunde, alipofungua kongamano la vijana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha siku ya kimataifa ya  vijana duniani.

Mavunde amesema vijana wanatakiwa kuwa wazalendo katika kuhakikisha wanalinda amani ya nchi na kuepuka watu ambao wana lengo la kuwatumia kufanya uchochezi.

Naibu huyo amesema kama taifa halitakuwa na amani ni wazi kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kufanyika.

Mbali na kuwataka vijana kulinda amani Mavunde aliwataka vijana kuachana na tabia ya kukaa vijiweni wakipiga soga za kuwasema wanasiasa au kushabikia timu za mpira kwa timu za ndani ya nchi au nje ya nchi.

“Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kukaa vijiweni wakibishania mambo ambayo hayana msingi wa kimaendeleo.

” Utakuta vijana wengi wa kitanzania wanatumia muda mwingi wakijadili timu ya mpira ya Asenol na Manchester au wanabishana kuhusu timu ya mpira ya Simba na Yanga badala ya kutumia muda huo kujadili nini wanaweza kufanya kwa maendeleo yao ya kujikwamua kimaisha”alisema Mavunde.

Katika kongamano hilo  Mavunde amewataka vijana kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ambayo itawawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wengine badala ya kusubiri ajira za serikali.

Mbali na hilo Mavunde amekemea tabia ya vijana ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kusambaza taarifa za uchochezi.

“Kutokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii,serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano TCRA wataendelea kuwafuatilia watu ambao wanasambaza taarifa za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya taifa” alisema Mavunde.

Naye mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN),Fatina Kiluvia, amesema vijana wanatakiwa kuimalisha amani zaidi sambamba na kujikwamua kimaisha.

Mwakilishi huyo amsema ili vijana waweze kujikwamua kimaisha ni lazima wawe wabunifu katika kuibua miradi ya kimaendeleo.

Kilele cha maadhimisho ya vijana kitaifa yatafanyika leo katika viwanja vya mwalimu Nyerere mjini hapa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Jennister Mhagama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!