Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Naibu Waziri awabebesha Wakurugenzi zigo la miradi chini ya kiwango
Afya

Naibu Waziri awabebesha Wakurugenzi zigo la miradi chini ya kiwango

Spread the love

IMEELEZWA kuwa usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo na ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali kwa baadhi ya halmshauri nchini unaotokana na baadhi ya wakurugenzi kushindwa kusimamia vizuri na kusababisha miradi mingi kujengwa chini ya kiwango huku ikitajwa kutumia fedha nyingi kuliko kawaida. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea). 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Februari 2023 na Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel, akiwa wilayani Momba katika ziara yake ya kikazi ya kupitia zahanati, vituo vya afya na hospitali zote kuangalia namna ya upatikanaji wa dawa ili serikali iweze kuongeza bajeti itakayokidhi mahitaji sahihi kwa wananchi.

Mollel amesema katika ziara iliyofanjwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa malalamiko mengi kwa wananchi yalikuwa ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea tiba huku wagonj wa wakienda kununua dawa kwenye maduka yanayomilikiwa na madaktari.

Alisema baada ya kumalizika ziara hiyo,ilimlazimu abaki ili avipitie vituo vyote mkoani Songwe na kupata idadi kamili ya mahitaji ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba na kudhibiti wizi ili serikali iweze kuongeza bajeti itakayokidhi mahitaji ya wananchi.

‘’Kitendo cha wananchi kununua dawa kwenye maduka yanayomilikiwa na madaktari kimewakwaza wananchi, na sasa baada ya mapitio Serikali itaongeza bajeti ya fedha kununua dawa na vifaa tiba hali itakayopelekea wananchi waache kununua dawa kwenye maduka hayo’,’ amesema Mollel.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel

Wakati huo akiwa wilaya ya Momba Naibu waziri Mollel,alishangaa kuona jengo la utawala lililojengwa kwa Sh 3.4 bilioni wakati wilaya zingine nchini jengo la aina hiyo hiyo limekuwa likitajwa kujengwa kwa Sh 5 bilioni na zaidi hali iliyomlazimu kuchukua ramani pamoja na BOQ.

Amesema amechukua ramani hiyo ili ikatumike kutoa semina elekezi kwa wakurugenzi wote nchini kuona na kujifunza namna ya matumizi sahihi ya fedha za miradi kama ilivyofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Momba, Regina Bieda aliyemshangaza hadi Waziri Mkuu.

“Mkurugenzi Bieda wa Momba anaweza kwenda kutoa semina kwa wakurugenzi wenzie nchini namna alivyoweza kutumia fedha ndogo kiasi hicho,” amesema Mollel.

Kwa upande wake Bieda amesema sababu kubwa ya kufanikisha hilo ni ufuatiliaji wa kila hatua katika manunuzi ya zana za ujenzi huku akiendesha vikao vya mara kwa mara na wakuu wa idara kuzungumzia mustakabali wa usimamizi wa miradi na ndiyo maana wamefanikiwa kufikia asilimia kubwa kabla ya muda uliowekwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!