Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Naibu Spika: Uongozi wa rais haupo sawasawa na kiongozi wa mhimili wowote
Habari za Siasa

Naibu Spika: Uongozi wa rais haupo sawasawa na kiongozi wa mhimili wowote

Spread the love

 

NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo uongozi wake haupo sawasawa na kiongozi yeyote wa mhimili wowote uliopo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Dk. Tulia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Januari, 2022 wakati akitoa salamu za pongezi kwa viongozi mbalimbali walioapishwa Ikulu jijini Dodoma.

Akizungumza kwa usisitizo, amesema kumekuwa na upotoshaji kuwa Rais ni kiongozi wa Serikali bila kutambua kuwa pia mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote.

“Sasa wapo watu wanachukua hiyo sehemu ambayo imesema rais ni kiongozi wa serikali, lakini Rais ana mambo yote ni mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali ni amiri jeshi mkuu nchi hii,” amesema.

Aidha, amesema Bunge lipo tayari kumpa ushirikiano Rais wetu pamoja na mawaziri wakiongozwa na waziri mkuu.

Amesema kwa mujibu wa katiba ni kazi ya Bunge kutunga sheria, kuishauri serikali na kuisimamia serikali.

“Sasa yako mazingira ambayo pengine kunatokea watu wakifikiri kazi ya Bunge kila wakati ni kuikosoa serikali, uko wakati ambao Bunge tunatakiwa kuishauri serikali, upo wakati bunge linatunga sheria, upo wakati ambao Bunge linaisimamia serikali.,” amesema

Amesema katika kipindi uongozi wa Rais Samia serikali iimekuwa ikisikiliza ushauri unaotolewa na wabunge pamoja na kuzifanyai kazi changamoto zinazotokea kwenye majimbo ya wabunge

“Kwa muktadha huo, Bunge lipo tayari kushirikiana na serikali ya awamu ya sita kwa mambo yote yatakayoletwa bungeni ili tuweze kutoa ushauri, tuisimamie serikali na kutungia sheria pale panapohitaji.

“Pale ambapo tutahitaji kuikosoa serikali itakosolewa kwa heshima lakini pia itakaosolewa kwa muktadha ambao Katiba inaturuhusu kufanya hivyo.

“Vivyo hivyo pale ambapo tunapaswa kuishauri serikali tutaishauri na lengo la kuishauri si kwamba serikali lazima ifuate ushauri wa Bunge ndio maana katiba hiyohiyo imetoa nafasi kwamba Bunge kuisimamia serikali hivyo linapata fursa ya kuiuliza serikali walifanyia ushauri gani ule ambao uliotolewa na Bunge au hapana,” amesema.

Pamoja na mambo mengine Dk. Tulia amewapongeza viongozi walioapishwa leo na kuongeza kuwa kila waziri aliyeteuliwa inawezekana ameshawahi kufanya kazi maeneo aliyopangiwa sasa.

“Ninawapongeza kwa sababu mnayo sehemu ya kuanzia kusema mazuri ya Serikali ya awamu ya sita na kazi nzuri ambayo Rais ameifanya kwa nchi hii.

“Niwape ushauri, niwaombe kwa sababu Rais amewaamini kumsaidia, hizo ni kazi zake na ninyi mnapozifanya fanyeni kama wasaidizi wa Rais Samia Suluhu na si vingine,” amesema.

1 Comment

  • Asante ndugu tulia tumekusikia ambao tulikuwa hatuelewi sasa tunaelewa kupitia maelezo yako tutafuata wako usia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!